HABARI MSETO (HEADER)


August 20, 2023

SINGIDA BIG STARS MGUU MMOJA NDANI CAF CC

Na John  Marwa

Klabu ya Singida Big Stars imetanguliza mguu mmoja mbele katika harakati za kuwania kutinga hatua ya awali kutinga makundi Kombe la Shirikisho Afrika CAF CC baada ya kuichakaza JKU mabao (4-1) katika Dimba la Azam Complex Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Ulikuwa mchezo wa mkondo wa kwanza hatua za awali, ambapo ni mchezo wa kwanza pia kwa Singida Big Stars kucheza michuano ya kimataifa tangu kuanzishwa kwake.

Ulikuwa mchezo mkali na wenye ushindani mkubwa kwa Singida kukitawala kipindi cha kwanza kwa kufanya mashambulizi ya kuhanikiza jambo lililopelekea kupata mabao mawili ya mapema kwa mikwaju ya penati baada ya walinzi wa JKU kufanya madhambi na kuunawa mpira ndani ya boksi kwa tafsiri ya mwamuzi.

Mikwaju yote miwili ya Singida Big Stars iliwekwa kimiani na nyota wao Marouf Tchakei, huku kiungo fundi Morice Chukwu akiipeleka Singida mapumziko kifua mbele kwa mabao (3-0) baada ya  kuachia kombora la masafa marefu 'Long Range Screemer'.

Kipindi cha pili JKU wakati hawajakaa sawa Duke Abuya aliachia shuti kali na kuiandikia Singida bao la 4. Baada ya bao hilo JKU waliamka na kaunza kujitetea kiasi cha kuwadhibiti Singida na presha hiyo iliifanya safi ya ulinzi ya Singida Big Stars na kuipeleka kupata mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Saleh Abdallah.

Bao hilo liliwapa JKU Nguvu za kuipelekea moto Singida kiasi cha kujikita wanakosa     utulivu na kufanya makosa mengi ambayo JKU walioshindwa kuwaadhibu Singida.

Kwa matokeo hayo Singida Big Stars wanasubiri mchezo wa marejeano wiki moja ijayo.




No comments:

Post a Comment

Pages