HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 01, 2023

GPE YAIPATIA TANZANIA DOLA ZA MAREKANI MILION 207 .3 KUBORESHA SEKTA YA ELIMU


Na Magrethy Katengu


TAASISI ya Ushirikiano wa Elimu Dunia ((GPE) imeipatia  Tanzania Dola za Marekani milioni 207.3 kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini ambapo matunda yake yanaonekana shule za Sekondari kujengwa kila kata pia Elimu Bure kuanzia shule za Msingi hadu Sekondari

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika hafla iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu Mkutano wa kuchangia fedha.za kuwezesha serikali katika sekta ya elimu ambapo GPE  imekuwa na mchango mkubwa Mwenyeki wa bodi ya GPE  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ampapo amesema fedha hizo zimetolewa kwa awamu mbili mwaka 2014/2018 na  2019 mpaka 2025.


Mwenyekiti wa Bodi ya GPE, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete katika hafla ya uchangiaji wa fedha za maboresho ya elimu nchini iliyohudhuriwa na. Wakuu wa. Mikoa. yote nchini ambapo amesema fedha hizo zimeelekezwa kwenye ujenzi wa madarasa, vyoo, nyumba za walimu na vifaa vya shule.maabara, ili kuchochea elimu ya Tanzania.


“watoto wa mjini wanasema kutoa kiwango  cha juu, GPE inatoa kiwango  cha juu  kwa kila dola moja ya Marekani itakayopatikana kupitia ufadhili wa sekta binafsi kama vile Kampuni, Asasi za Kiraia au Mabenki, Taasisi ya GPE nayo itatoa Dola moja ya Marekani kwa kila shilingi moja " amesema Rais Mstaafu.

“Mkichangia nyingi, GPE inatoa nyingi, mkichangia kidogo GPE itatoa kidogo, lakini pia kwa kila Dola 3 za Marekani zitakazotolewa kama msaada au msamaha wa Kodi, kutoka taasisi za fedha za Kimataifa, au nchi Washirika wa Maendeleo, Taasisi ya GPE nayo inatoa Dola moja.”Amesema Kikwete na kuongeza kuwa “Pia kama nchi ina mikopo IMF nchi ikifanikiwa kuongea na anayewadai kwa kila Dola 3 inayosamehewa, GPE inachangia Dola 3 kwa masharti ya fedha zinazosamehewa kuingizwa kwenye sekta ya elimu.

“Mfano, mnafanya mazungumzo na Uingereza bwana tusamehe deni hili, hizo fedha ambazo tungekulipa wewe hizo pesa tutazitumia Kwa ajili ya elimu.
 

“Uingereza iseme tunawasamehe Dola 10,000 Kwa masharti kwamba muelekeze kwenye elimu, ukishapata huo msamaha GPE kwa kila Dola 3 inachangia wao. ”
Kikwete na kufafanua zaidi

Utaratibu huu wa kibunifu unalenga kupatikana fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu na kuongeza uwekezaji, kutoa fursa kwa wadau kushirikiana kwa  pamoja kuendeleza sekta ya elimu.

Amesema GPE ni Shirika lililoanzishwa miaka 20 iliyopita na mataifa saba makubwa duniani sio Shirika jipya shabaha yake ni kusaidia elimu katika nchi za kipato cha chini na hadi sasa inasaidia nchi 88 na Tanzania ni Miongoni mwa nchi nufaika

Hata hivyo Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa walioahidi kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 465 kama ahadi ambazo zitaisaidia nchi kupata fedha za ruzuku (grant) kiasi cha Dola milioni 50.

“tumeshasikia jinsi ahadi zilivyotolewa, zaidi ya shilingi Bilioni 465, matumaini yangu walioahidi watatoa, ahadi ni deni, Wakuu wa Mikoa mmetoa ahadi wenyewe hapa” amesema Mheshimiwa Jakaya Kikwete.

Aidha, Kikwete amesema miradi ya GPE nchini, ilifadhiliwa kwa awamu mbili za mwaka 2014 hadi 2018 na 2018 hadi 2023 ikihusisha ujenzi wa madarasa mapya ya shule za msingi 2,980, mabweni ya wanafunzi wenye mahitaji maalum 14, matundu ya vyoo 7,673, shule mpya 98, shule mpya 18, nyumba za walimu 94, ukarabati wa vituo vya walimu 13 (TRC), ujenzi na uendeshaji wa vituo vya walimu 12, uendeshaji wa Mafunzo ya Walimu Kazini (MEWAKA) na ununuzi wa vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia kwa walimu na wanafunzi.

Awali Prof. Adolf Mkenda akimkaribisha mgeni rasmi amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amejenga imani kubwa kwa Sekta Binafsi nchini na ndio maana Wadau wameitikia kwa kiwango kikubwa na kuendelea kutoa michango yao kwenye elimu hapa nchini na hivyo ni jambo jema kwa wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais TAMISEMI kutambua mchango wa Wadau kwenye Sekta ya Elimu nchini.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Adolf Ndunguru ametoa rai kwa Wakuu wa Mikoa kuweka utaratibu mzuri wa usimamizi wa utekelezaji wa ahadi zilizowekwa na Wadau, kuanzisha ‘Kanzidata’ kwa kila mkoa ili kurahisisha ufuatiliaji na tathmini ya ahadi zilizotolewa lakini pia kuendelea kuwaelimisha Wadau kwa kuwa zoezi hilo ni endelevu.

Mpaka sasa Washirika wa GPE Duniani wanatoa msaada wa kifedha kwa nchi 88 ili kuinua Sekta ya elimu na kutimiza lengo la kutomuacha nyuma mtoto yeyote katika kupata haki ya elimu.

Katika ahadi zilizotolewa mkoa wa Mara umeibuka kidedea kwa kutoa ahadi ya Shilingi Bilioni 155 wakati Dar es Salaam ukiahidi kutoa Shilingi Bilioni 20.


No comments:

Post a Comment

Pages