HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 01, 2023

UWT RUVUMA WAMPONGEZA MBUNGE MARIAM NYOKA KWA UJENZI WA CHOO NA KUTOA MISAADA YA MILIONI 24.5 MBINGA

NA STEPHANO MANGO, MBINGA

 

UONGOZI wa Umoja wa Jumuiya ya Wanawake w UWT Mkoani Ruvuma umempongeza Mbunge wa Viti Maalum Mkoa huo Mariam Madalu Nyoka kwa kujenga choo chenye matundu sita cha Club ya Manzese Wilaya Mbinga na kutoa vifaa vya usafi jumla ya milioni 10.2


 

Akizungumza kwenye halfa ya kukabidhi msaada wa choo hicho Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Eliza Ngongi alisema kuwa Jumuiya hiyo inampongeza sana Mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi zake mara kwa mara.

Ngongi alisema kuwa nimezunguka Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma nikiwa na Mbunge Nyoka nimeona akiahidi na kutekeleza ahadi zake kwa vitendo, jambo ambalo linaonyesha umakini na uweredi katika uwakilishi

"Natoa Shukruni kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Mariam Nyoka kwa kuwa mmoja wa Viongozi ambao michango na misaada yao kwa Jamii inaonyesha wazi Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025" alisema Ngongi.


 

Uongozi umesema kuwa hatua aliyochukua Mbunge Nyoka ni nzuri kwani imethibitisha ni kwa kiwango gani anaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mbunge Mariam Madalu Nyoka alisema kuwa ndani ya miezi 3 toka mei hadi Agosti mwaka huu kwa Wilaya ya Mbinga tu ametumia  jumla ya fedha milioni  24,573,000. Kwa ajiri ya kutoa misaada mbalimbali

Alisema kuwa pamoja na kukijenga choo hicho na kukikabidhi kwa wajasiliamali ambao wanafanya shughuli zao kwenye soko hilo pia amefanikiwa kununua  geti la kituo cha watoto yatima St. Vicent mbinga milion 2

Nyoka alisema kuwa watoto hao pia amefanikiwa kuwapatia mahitaji mbalimbali ikiwemo  mablanket 70, mashuka 45, sabuni, mafuta sukari kg.50, sabuni caton 3 baby shoo 5,

Alisema kuwa kwa upande wa Wajasiriamali wajane (Waviu) aliwapatia mtaji wa mahindi wa milioni 2, pia alichangia ujenzi wa Ofisi ya Ccm Wilaya Mbinga Cement mifuko 100 yenye thamani ya 1,700,000,

Katika kuendelea kuwainua Wajasiriamali wadogo sana wenye mitaji chini ya 5000, aliwaongezea mtaji kila mmoja 15,000 idadi yao ni 72 ambapo jumla ya milioni 1,080,000, aliwapatia

Aidha ametoa  viti mwendo kwa watu wenye ulemavu 2, mashuka ya Wagonjwa 40, mashine za kupima presha 2, kupima sukari mashine 2, neti za vitanda vya wagonjwa 30 katika Hospitari ya Mbuyula Mbinga na kuwezesha vikundi 7 vya  kilimo cha maharage, mahindi na wahoka mikate kila kimoja kilipewa shilingi 500,000 na kufanya jumla ya milioni 3,500,000./=

No comments:

Post a Comment

Pages