HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 12, 2023

Koka atekeleza ahadi zake kwa vitendo soko la mnarani

Na Victor Masangu, Kibaha


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ametekeleza ahadi yake kwa vitendo kwa wafanyabiashara wa soko la mnalani kwa kuwakabidhi matenki makubwa matatu kwa ajili ya kuhifadhia maji.

Koka amekabidhi matanki hayo wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuweza kuwatembelea na kuzungumza na wafanyabiashara wa bidhaa  mbali mbali ikiwa sambamba na kutekeleza ahadi zake ambazo aliziahidi kipindi cha nyuma.


Aidha katika ziara hiyo Mbunge Koka ambaye aliambatana na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nikson Saimon pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kibaha Mussa Ndomba.

Mbunge huyo alisema kwamba ana imani kwamba matanki hayo ya maji yataweza kuwasaidia  kwa kiasi kikubwa kupunguza kero na adha ambayo ilikuwa ikiwakabili wafanyabiashara hao kwa kipindi cha muda mrefu.

Sambamba na hilo Koka amekabidhi televisheni (TV) mbili za kisasa  zenye ukunbwa wa nchi 45 kwa lengo la kuwapa guess ya wafanyabiashara hao kutazama na  kupata  matukio na taarifa  mbali mbali kutoka   ndani na nje ya nchi.

"Kipindi cha nyuma nilipita katika soko hili na niliahidi matanki ya maji makubwa matatu.,Televisheni mbili sambamba na vifaa vya michezo ikiwemo mipira pamoja na jezi na leo hii nimekuja rasmi kwa ajili ya kuvikabidhi,alisema Koka.

Aidha Mbunge huyo aliongeza kwamba lengo lake kubwa ni kuwawekea mazingira mazuri wafanyabiashara hao ili soko liweze kuwa la kisasa zaidi na waweze kufanya biashara zao katika mazingira ambayo ni rafiki.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nikson Saimon alimshukuru kwa dhati Mbunge huyo kwa kuweza kuona umuhimu wa kuwasaidia wafanyabiashara hao na kwamba serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuendelea kuboresha miundombinu ya soko hilo.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Mussa Ndomba alibainisha kuwa kwa sasa wameshatenga zaidi ya milioni 200 kwa ajili ya kuezeka paaa katika soko hilo ili kuondokana na changamoto hasa katika kipindi cha mvua kwani bidhaa zimekuwa zikilowa.


Nao baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wamempongeza Mbunge huyo kwa kuweza kutekeleza ahadi yake kwa vitendo na kwamba matanki ya maji waliyopatiwa yatakuwa ni mkombozi mkubwa wa upande wao katika kuhifadhi maji.


No comments:

Post a Comment

Pages