HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 12, 2023

TRA Ilala yazindua Kampeni kuhamasisha Matumizi EFD

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Ilala mkoani Dar es Salaam Masau Malima amesema kutoa na kudai risiti  sahihi za EFD  inasaidia kukusanya kodi stahiki kwa maendeleo ya taifa.

Akizungumza jijini humo wakati wa Kampeni ya TUWAJIBIKE ya uhamasishaji wa  matumizi sahihi ya EFD uliofanyika Kituo cha huduma za kodi Gongolamboto Malima amesema kodi yetu ndiyo maendeleo yetu" hivyo  amewahimiza wafanyabiashara kutoa risiti kila wanapofanya mauzo.

Pia wanunuzi kudai risiti sahihi za EFD kila wanaponunua bidhaa au kupata huduma. Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha huduma za kodi Gongolamboto wilayani Ilala.

Kwa  upande  wake Mkuu wa Kituo cha Kodi Gongolamboto Ambele Mwaisunga amewakaribisha wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kufika katika kituo hicho kupata huduma zinazohusiana na masuala ya kodi.

 "Tunawakaribisha wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kufika katika kituo chetu cha huduma Gongolamboto". Pia amesema huduma za TRA kwa sasa zimesogezwa karibu na wafanyabiashara katika maeneo yao ya biashara hivyo wasisite kufika na kupata huduma mbalimbali za kodi. 

Aidha wafanyabiashara wameipongeza TRA kwa kusogeza huduma karibu na maeneo yao hivyo kupunguza gharama na muda wa kupata huduma za kodi pia wameishukuru TRA kwa kuendelea kuwakumbusha wafanyabiashara hao wajibu wao juu ya mambo mbalimbali ya kikodi ikiwemo kutoa na kudai risiti.

No comments:

Post a Comment

Pages