HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 29, 2023

RAIS RT AISHUKIA ARUSHA KUSUSIA MASHINDANO YA TAIFA

*Awataka viongozi wake wajitathmini, hatua kuchukukuliwa


Rais RT, Silas Isangi (wa pili kulia), akifuatilia mashindano ya Taifa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


NA TULLO CHAMBO, RT


RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Silas Isangi, amewashukia viongozi wa vyama vya mikoa iliyoshindwa kuleta timu kwenye mashindano ya Taifa wakiongozwa na Arusha huku akibainisha kuwa wanaoathirika ni wachezaji.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, mbali na kuipongeza mikoa iliyojitokeza kushiriki, huku akionyeshwa kukerwa na Arusha, ambao alibainisha wameandika barua wakidai mashindano hayo yamepitwa na muda.


"Ingekuwa ni uchaguzi au mkutano mkuu, viongozi hao wa mikoa wangekuwa hapa, lakini kwenye mashindano ya taifa hawajaleta timu, wanaoathirika ni wacheza na wala sio hapo viongozi...kama wanaona hawawezi wapishe watu wengine waongoze, hili tutalishughulikia," alisisitiza na kuongeza.


Mbio hivu sasa ni pesa, mchezaji unapofanya vizuri unajitengeneza rekodi, unanufaika na kuiletea nchi yako sifa, mnapaswa kufuata nyayo za kina Bayi (Filbert bingwa wa zamani wa dunia wa mita 1500.


Mgeni Rasmi, Charles Maguzu ofisa kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) aliyemwakilisha Katibu Mtendaji, Neema Msitha, aliwataka wachezaji kuyatumia mashindano ya taifa kuimarisha muda wao kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.

Kwa upande wa waliosusia, alieleza kuwa yana umuhimu mkubwa kwa wachezaji, kwani yanawapa fursa ya kujipima na kujiandaa kwa mashindano ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Pages