HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 06, 2023

Tatizo la upatikanaji wa Dola kupungua - Chalamila

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema kuwa kufanyika kwa mkutano wa Jukwaa la Mifumo hapa nchini kunaweza kusababisha kupunguza tatizo la dola ambalo lilikuwepo kwani  Dola inapokuja nchini inapunguza tatizo hilo.

Amesema kuwa hata kwa upande wa vyakula na Tanznaia itaweza kufaidika na hasa kwa upande wa Dar es Salaam na kwamba ikifaidika Dar es Salaam manaake nchi imefaidika kwani mkoa huo ndio kitovu cha uchumi wa nchi .

Chalamila ametoa kauli hii leo Septemba 4, 2023  kwenye viwanja vya kituo cha mikutano ya kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ambapo Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula unafanyika.

Amesema kuwa Dar es Salaam ndio Kila kitu kwani kuna wakazi si chini ya milioni tano na ndio kitovu cha masuala mengine yote yanayohusu biashara za kawaida za ndani na nje  na zaidi nikwamba Dar es Salaam itafaidika sana Kutokana na utalii utakaokuwa unafanya na wageni mbalimbali we aliokuja kwenye mkutano huo.

Chalamila amesema kuwa kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuja kwenye mkutano huo hadie ukumbi wa Mwalimu Nyerere unaonekana ni mdogo na katika hili inapelekea kupata mawazo ya kuongeza kumbi zingine  na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameshaliona hilo na mapema sana ukumbi huo utaaza kupanuliwa Ili kukidhi mahitaji makubwa ya matumizi.

Ameongeza kuwa mkutano huo ni miobgoni mwa mkutano mkubwa ambao unafanyika katika ukanda huu na Kuna mkutano mungine mkubwa wa shirikisho wa michezo Dunia  nao utafanyikia hapa na mkutano huo mambo yakiwa tayari utatangazwa hasa baada ya Rais Dkt. Samia kuwaongoza juu ya mkutano huo .

Amesema kuwa kupitia mkutano huo ambao unatarajia kufanyika hapa nchini tayari vyumba vineshaaza kubukiwa  na wito wake Kwa wakazi wa Dar es Salaam nikwamba fursa kama hizo haziji mara mbili hivyo wajaribi kutumia fursa hiyo vizuri ili kuweza kupata faida za mkutano huo mkubwa na kuweza kuuutumia vizuri.

Amesema kuwa mkoa wa Dar es salaam uko salama na hali Iko Shwari na Ulinzi uko Kwa asilimia 100 na hakuna mtu yeyote ambaye atapata itilafu katika kuisho hapa Dar es salaam kuazia Leo hadi utakapotamatika.

Akizungumzia Kwa upande wa vijana amesema kuwa hivi Sasa kilimo sio tena adhabu hivi Sasa mh.rais  Dkt Samia ameleta kilimo kama biashara, fursa, kilimo ni sayansi hivyo vijana waliomaliza vyuo vikuu na ambao hawajamaliza watumie fursa hiyo vizuri na watende Kwa vitendo na waifutilie kweli kweli ili kuweza Kubadilisha maisha.


No comments:

Post a Comment

Pages