HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 06, 2023

Kocha Mkuu Singida Fountain Gate FC kuja na wasaidizi wake

Ujio wa Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate FC, ambayo imeweka kambi jijinj Dar es Salaam kujiandaa na hatua ya pili ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) Kocha Msaidizi, Mathias Lule amebaki Singida na kudai hatokuwa sehemu ya benchi hilo la ufundi.

Kocha Lule hayuko sehemu ya benchi la ufundi ambalo limesafiri na timu hiyo  hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa Shirikisho Afrika dhidi ya Future FC ya Misri, ambao utafanyika Jumapili ya Septemba 17, mwaka huu, uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya timu hiyo zinaeleza kuwa baada ya ujio wa kocha mpya  Ernest Middendorp ambaye anahitaji kufanya kazi na watu wake ambao aliwahi kuwa nao awali kabla ya kutua hapa nchini.

Mtoa habari huyo amesema Kocha Middendorp amewaeleza viongozi wa timu hiyo kuwahitaji watu wake wakufanya nae kazi ikiwemo kocha msaidizi na hata kocha wa makipa ambapo jambo hilo linafanyiwa kazi.

“Ni kweli kutakuwa na mabadiliko ya benchi la ufundi kwa sababu kocha mpya, Middendorp anahitaji kufanya kazi na msaidizi wake, jambo hilo limepelekea kocha Lule kupangiwa majukumu mengine ndani ya timu hiyo na kutoambatana na timu hiyo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kimataifa,” amesema mtoa habari huyo.

Hata hivyo alipotafutwa Kocha Lule amekiri  kutokuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu  iliyopo Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya kombe la Shirikisho kwa sababu yuko Singida kwa ajili ya majukumu mengine.

“Ni kweli sijaondoka na timu iliyopo Dar es Salaam, niko Singida nikifanya majukumu mengine ya timu, suala la kuondolewa kwenye timu sifahamu kwa sababu bado nina mkataba na Singida Fountain Gate FC ,” amesema Lule.

No comments:

Post a Comment

Pages