WANARIADHA wa Tanzania wametamba katika mbio za NAGAI City Marathon zilizofanyika jijini Nagai nchini Japan, Oktoba 15, 2023.
Mwanariadha Sara Ramadhan aliibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake Km. 42 'Full Marathon' huku pia kwa wanaume Peter Sulle akishinda na kufuatiwa na Fabian Joseph.
Watanzania pia walifanya kweli kwenye Km. 21 'Half Marathon', ambako kwa
Wanawake Transfora Musa aliibuka kidedea.
Kwa upande wa Wanaume, ilishuhudiwa Josephat Gisemo akiibuka mshindi wa kwanza na kufuatiwa na Paul Damian Makiya.
Tanzania iliwakilishwa na wanariadha sita katika mbio hizo, wakiwa chini ya Kocha Samson Ramadhan na Mkuu wa msafara Kanali mstaafu Juma Ikangaa.
No comments:
Post a Comment