HABARI MSETO (HEADER)


October 15, 2023

KIKOSI CHANGU KITAFANYA VIZURI KATIKA MASHINDANO YA CAF

ROBERTINHO KOCHA Mkuu wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amefunguka kuwa, amefuatilia timu anazokutana nazo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kudai anaamini kikosi chake kitafanya vizuri kwa kuwafunga wote.


Katika michuano hiyo, Simba imepangwa Kundi B na timu za Wydad Casablanca ya Morocco, ASEC Mimosas (Ivory Coast) na Jwaneng Gallaxy (Botswana).


Mechi za hatua ya makundi zinatarajiwa kuanza kati ya Novemba 24 na 25, mwaka huu ambapo kila timu lazima zikutane mara mbili nyumbani na ugenini, kisha zile mbili za juu zitafuzu 16 bora pindi hatua ya makundi ikikamilika.


Robertinho amesema kuwa, Simba ni miongoni mwa timu kubwa Afrika, hivyo wana furaha kucheza mechi ngumu kama hizi za Ligi ya Mabingwa Afrika. Kocha huyo alisisitiza kuwa, kwenye kikosi chake, kuna wachezaji wenye kiwango kizuri na anaendelea kuwasuka vijana wake kupata matokeo mazuri zaidi nyumbani na ugenini.


Tuna mikakati mizuri kuelekea mechi hizo, katika histori Simba iliwahi kucheza na timu zote, ikiwemo Wydad Casablanca ambayo hapa tulipata matokeo mazuri nyumbani na kwenda kupoteza ugenini."


"Kazi kubwa kwa sasa ni kuandaa timu ambayo itapata matokeo mazuri nyumbani na ugenini ili kutafuta alama za kwenda hatua ya robo fainali ya Afrika."

No comments:

Post a Comment

Pages