Dar es Salaam, Tanzania
Wakati
maandalizi ya Ibada ya Hija Halisi ya mwaka huu yakizidi kupamba moto
kwa wengi kuendelea kujisajili kuungana na maelfu ya waliokwishajisajili
kwenda Kigoma kwenye Hija hiyo, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba
Halisi amesisitiza kuwa Hija hiyo siyo ya kukosa kwa sababu ni ya kwenda
kupata Baraka na utajiri tele kutoka kwa CHANZO HALISI na siyo kutalii.
Baba
Halisi ametoa msisitizo huo jana Jumapili 12 Thebeti, 1 Majira HalisiI
au Disemba 17, 2023 kwa Kalenda ya Gregory, katika Ibada iliyofanyika
Makao Makuu ya Kanisa Halisi la MUNGU BABA, Tegeta - Namanga, Jijini Dar
es Salaam na kuhudhuria na mamia ya watu wakiwemo Watekeleza Sauti,
Uzao na watu wengine mbalimbali.
Kwa mujibu wa Baba Halisi jana
lilikuwa lango ambalo Waabuduo Halisi walipatikana, hivyo iliambatana na
sherehe ambapo Baba Halisi alitoa makreti kwa makreti ya vinywaji
baridi (soda), na kuhakikisha kila yeyote aliyekuwepo kwenye ibada hiyo
anakunywa hadi kutosheka.
Baada ya Baba Halisi kuachilia somo la
WAABUDUO HALISI TUMEPATIKANA katia Ibada hiyo ndipo, akahitimisha kwa
kuzungumzia habari ya Hija Halisi ambayo itafanyika Disemba 31, 2023,
ambayo kwa Kalenda inayofuatwa na Kanisa Halisi itakuwa ni Jumapili, 26
Thebeti 1 Majira Halisi.
"Mimi siyo kichaa, ninapoisisitiza kila
mtu asiikose Hija hii ninamaanisha. Pale tunaenda kushukuru Utimilifu wa
Matahayo 21:43, katika ule Yesu zaidi ya miaka 2000 baada ya Wayahudi
kumkataa alisema Ufalme utahama kutoka Mashariki ya Kati kwenda Taifa
lingine ambalo kwa wakati ule hakulitaja. Sasa baada ya Sauti kusikika
mara nne Kigoma, tunaenda kushukuru kujua kumbe Taifa lenyewe ni
Tanzania. Na siyo tu kushukuru bali pia tunaenda kupokea Utajiri na
Baraka za CHANZO HALISI ", akasisisitiza Baba Halisi.
Ibada kama
hiyo ya Hija ambayo hufanyika kila mwaka tangu Kanisa Halisi
lilipoasisiwa hapa nchini tariban miaka sita sasa, ilifanyika Kigoma
mjini, Januari 29, 2023 sawa na 26 Thebeti 1Majira Halisi, na
kuhudhuriwa na maelfu ya mahujaji kutoka ndani na nje ya Tanzania, Mgeni
Rasmi akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji Fredinand
Filimbi ambaye alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kigoma.
Baadhi ya
Mahujaji wa Hija hiyo walitoka mikoa yote ya Tanzania Bara, Zanzibar,
Marekani, Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi, Malawi na Msumbiji na
kushiriki hatua kwa hatua Ibada hiyo mwanzo hadi mwisho, huku wote
wakionyesha kuwa wachangamfu tena wenye furaha.
Ibada ya mwaka
huu (kwa Kalenda ya Majira Halisi kabla ya Uharibifu) itakuwa ni ya sita
(6), na inatarajiwa kuwa ya 'kukata na shoka' kwa sababu, mbali na
mahujaji ambao ni Uzao Halisi lakini pia wanatarajiwa kushiriki Wazee
zaidi ya 40 wakiwemo wa kutoka Baraza la Wazee mkoa wa Dar es Salaam
wakiongozwa na Mwenyekiti wa baraza hilo Mzee Mohamed Mtulia na Wazee
kutoka mkoa wa Njombe.
Tazama picha za Ibada ya 'Waabuduo Halisi tumepatikana'.👇
Baba Halisi, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la MUNGU BABA akiachilia somo la'Waabuduo Halisi tumepatikana' karika Ibada iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, 12 Thebeti, 1 Majira HalisiI (Jumapili Disemba 17, 2023).
Mwazo
Moja Halisi akiamkaribisha Baba Halisi wakati akiondoka Utajirishoni.
Baba Halisi akiwa tayari utajirishoni huku akionesha kuwa mwenye furaha tele.
'Mtekeleza Sauti' kutoka Star Tv akimualika Baba Halisi kuanza kuongoza Ibada hiyo.
Baba Halisi akianza kuongoza Ibada hiyo kwa kuongoza Shukurani. Kulia ni Mnara Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi wakipokea Shukurani hiyo.
Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao Halisi wakiwa kwenye Ibada hiyo. Kulia ni Mtekeleza Sauti kutoka Vingunguti Thebeti Halisi.
Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao Halisi wakiwa kwenye Ibada hiyo.Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao Halisi wakiwa kwenye Ibada hiyo.Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao Halisi wakiwa kwenye Ibada hiyo.Baba Halisi akiomba nyimbo mbili zipigwe kabla ya kuendelea kuongoza Ibada hiyo.
Mwimbaji akiongoza kuimba wimbo kama alivyoomba Baba Halisi.
Wacharaza gitaa wakikoleza wimbo huo.
Baba Halisi akifuatilia wakati wimbo aliotaka ukipigwa.Mwimbaji Uelewa wa Sauti ambaye amejiunga na hivi karibu na Bendi ya Kanisa Halisi akiimba wimbo wa pili wa Hija Halisi Kigoma.
Watekeleza sauti na uzao wakicheza wimbo huo.
Uelewa wa Sauti akikoleza wimbo huo. |
Uzao wakicheza wimbo huo.
Baba Halisi akiruka kuucheza wimo huo.
Mama Halisi akicheza wimbo huo pamoja na Mnara Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi.
Mama Halisi, Mnana Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi wakifurahia wimbo huo.
Kisha Baba Halisi akabariki Maji kuwa Damu Safi ya Chanzo Halisi kuyaongozea Ibada hiyo.
Mama Halisi, Moja Halisi, Kanisa wa Uzao Halisi na Kanisa wa Fahari Halisi wakiwa na maji wakati Baba Halisi akiyageuza kuwa Damu safi nyeupe ya Chanzo Halisi.
Akiwaonyesha Uzao Damu safi ya Chanzo Halisi baada ya kuyabariki.
Akayanywa.
'Mtekeleza Sauti' kutoka Star Tv naye akanywa aliyokuwanayo.
Baba Halisi akinyunyiza Damu safi nyeupe kuzunguka Utajirisho.
Mama Halisi akigawa Maji kwa uzao baada ya kuelekezwa na Baba Halisi.
Mama Halisi akigawa Maji kwa uzao baada ya kuelekezwa na Baba Halisi.Moja Halisi akigawa Maji kwa uzao baada ya kuelekezwa na Baba Halisi.Moja Halisi akisoma Kitabu kufafanua kwa nini Baba Halisi anasema 'Waabuduo Halisi tumepatikana'. walikuwa hawakuweza kupatikana nyakati zilizopita.
Moja Halisi akisoma Kitabu kufafanua kwa nini sasa Baba Halisi anasema 'Waabuduo Halisi tumepatikana'.Baba Halisi akieleza Waabuduo Halisiwamepatikanaje sasa.
Watekeleza Sauti wakipanga kreti za soda kabla ya kugawa soda Uzao na kila aliyekuwepo apewe kwa ajili ya kunywa kusherehekea 'Waabuduo Halisi tumepatikana'.Uzao wakijipanga kupokea soda mmoja baada ya mwingine, huku wakitoa matunda.
Baba Halisi akiwa ametulia wakati ugawaji soda ukiendelea.
Fahari Halisi na Kanisa wake wakiwa wametulia wakati ugawaji soda ukiendelea.
Mama Halis, Mnara Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi wakiwa wametulia wakati ugawaji soda ukiendelea.
Uzao wakiendelea kutoa matunda.Baba Halisi akiongoza shukurani baada ya ugawaji wa soda.
Wakipokea shukurani.
Wakipokea shukurani.
Wakipokea shukurani. Wapili kushoto Dk. Yatosha kutoka Dawati la Polisi la Usalama na Amani katika Jamii.
Baba Halisi akihitimisha Ibada kwa kunyunyiza damu safi nyeupe ya Chanzo Halisi.
Moja Halisi akibarikia Kichanga.
Baba Halisi akikituza noti kichanga hicho.
Faida Halisi na Moja Halisi wakisimamia wakati Uzao wakijiandikisha kwenye dawati la Hija ili kwenda Hija Halisi Kigoma.
Mwimbaji akiimba wimbo wa Hija.
Baba Halisi akieleza umhimu wa Hija, na kuwamihiza Uzao kuhakikisha kila mmoja hakosi kwenda Hija hiyo ya mwaka huu.
Mwimbaji akiongoza wimbo wa Hija.
Mama Halisi, Mnara Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi akifurahia wimbo huo.
Baba Halisi akiendelea na hatua za mwisho za Ibada hiyo.
Baba Halisi akiwatakia heri uzao waliokuwa Ibadani na waliokuwa wakifuatilia Ibada hiyo katika Luninga na mitandao ya Kijamii.
Baba Halisi akiondoka Baada ya kuhitimisha Ibada hiyo.
Mnara Mmoja Halisi akafuatia kuondoka.
Udhihirisho Halisi akafuatia kuondoka.
Picha za ziada👇
Mtekeleza sauti wa Uzalishaji (kushoto) akizungumza na 'Mtekeleza Sauti kutoka Star Tv.
Uzao Halisi akipendeza ndani ya fulana la 'Bila Chanzo Halisi Hutoboi'.
No comments:
Post a Comment