HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 19, 2023

FCS YATOA TATHIMINI YA MWAKA MMOJA UTEKELEZAJI MRADI WA 'URAIA WETU'

Msimamizi wa Mradi wa 'Uraia Wetu' Nicholas Lekule akitoa tathimini juu ya Mradi huo, katika semina ya Wahariri na Waandishi wa Habari iliyofanyika leo Disemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.

Msimamizi wa Mradi wa 'Uraia Wetu' Nicholas Lekule akizungumza kwenye Mahojiano na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo, Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa MTWANGO NET Fidea Ruanda, akitoa wasilisho juu ya tathimini ya Mradi huo katika semina hiyo Jijini Dar es Salaam.

 

DAR ES SALAAM 

Foundation For Civil Society (FCS), kupitia mradi wake wa 'Uraia Wetu' imeendelea kuweka nia ya kuchangia, kuboresha, na kuwezesha mfumo wa sera na mazingira ya ushirikishwaji wa wananchi ili kukuza utawala wa Demokrasia nchini.

Malengo makubwa ya Mradi huo ni kukuza uhuru wa kujieleza, kupata habari, uhuru wa kukusanyika na kubaini fursa na nafasi iliyopo kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika masuala ya kiraia.


Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa Mradi wa 'Uraia Wetu' Nicholas Lekule, alipokuwa akitoa tathimini juu ya Mradi huo katika semina ya Wahariri na Waandishi wa Habari iliyofanyika leo Disemba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.

"Lengo la mradi huu wa miaka mitatu, ni kuwa asasi za kiraia ambazo zimeratibiwa vizuri kuanzia katika masuala ya kisheria, kisera na utekelezaji, ili kazi zinazofanywa ziwe na ufanisi mzuri" amesema Lekule.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa MTWANGO NET Fidea Ruanda, ameishukuru FCS kwa kutoa ruzuku ya kutekeleza Mradi huo wanaotekeleza kwa miaka mitatu katika mikoa saba ikiwemo Songwe, Ruvuma, Iringa, Njombe, Mbeya, Mtwara, Rukwa, ambapo wanasimamia Kanda ya kusini na kwamba unaolenga kuwajengea uwezo vijana, wanawake, na walemavu.


"Uwelewa mdogo kuhusu sera, sheria na miongozo mbalimbali ikiwemo kulipa ada kwa mashirika machanga bado ni changamoto licha ya kuwa malipo ni shilingi 50,000 kwa mwaka kwani usipolipa hadi kufikia mwezi wa April mwaka unaofuata unapigwa faini asilimia 100 ambapo ni sawa na shilingi 100,000" amesema Fidea.

No comments:

Post a Comment

Pages