Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete akizungumza leo na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha ( ATC) ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya mfumo wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma kutika Chuo Ufundi Arusha ( ATC) yaliyofanyika katika Chuoni hicho.
Mkurugenzi wa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora ambaye pia ni Mwezeshaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma, Bi. Leila Mavika akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa na Mkuu wa Chuo cha Arusha( ATC) Dkt.Musa Chacha wakiangalia baadhi ya mashine za kufundishia wanafunzi kwa vitendo katika chuo hicho kilichopo Jijini Arusha.
Na Lusungu Helela- Arusha
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe.Ridhiwani Kikwete amesema matumizi ya mfumo wa PIPIMS, PEPMIS na HR
Assessment katika Utumishi wa Umma nchini itaimarisha Utumishi wa Umma
kwa kuwabana Watumishi wanaopenda kukaa ofisini pasipo kufanya kazi.
Mhe.Kikwete
ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha wakati akizungumza kwa nyakati
tofauti na Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano cha Arusha ( AICC) na Chuo cha Ufundi Arusha
ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mafunzo ya
matumizi ya Mfumo wa Kupima Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma na
Taasisi (PEPMIS na PIPMIS) na Mfumo Maalum wa Tathmini ya hali ya
Rasilimaliwatu Serikalini (HR Assessment).
Amesema
Serikali imedhamiria kuimarisha Utumishi wa Umma kwa kuhimiza
uwajibikaji ili kuhakikisha kama Taifa linakuwa na utumishi wa umma
unaopimika kwa kumpima Mtumishi mmoja mmoja pamoja na Taasisi kwa
ujumla.
Ameongeza
kuwa mfumo wa PEPMIS umekuja kuwa mbadala wa OPRAS ikiwa ni utekelezaji
wa agizo la Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayelenga kuimarisha
mifumo ya uwajibikaji inayowezesha viongozi na watumishi wa umma
kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wakati na mahali popote.
Katika
hatua nyingine Mhe. Kikwete amewataka Maafisa Utumishi na Maafisa
Tawala kuacha kukaa ofisini badala yake waende maeneo ya kazi ili
kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi walio chini yao.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.John Mongela amesema zama hizi
hazihitaji watu wenye misuli kutokana na kukua na teknolojia. Hivyo,
teknolojia imerahisisha utendaji kazi na sisi tuko tayari kuisimamia
utekelezaji wake.
Amesema
ujio wa mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo Maafisa Utumishi
na Maafisa Tawala wataanza kubadilika na kuachana na utaratibu wa
kizamani wa utendaji kazi wao.
Hata
hivyo ametumia fursa hiyo kuiomba Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala
Bora kuwanoa upya Maafisa Utumishi na Maafisa Utawala wa mikoa na
Halmashauri kwani utendaji wao wa kazi sio wa kuridhisha ikizingatiwa
wao ndo wenye jukumu la kuwasimamia watumishi wengine.
No comments:
Post a Comment