Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Mitawi (katikati) akizungumza kwenye kikao cha mwaka cha Kikundi kazi cha Kilimo endelevu na jumuishi cha SAGCOT (GRG) kilichofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bw. Jabiri Makame, watatu Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Bw. Geophrey Kirenga na wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mvumelo Bi. Judith Nguli.
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Mitawi (kushoto) akizungumza kwenye kikao cha mwaka cha Kikundi kazi cha Kilimo endelevu na jumuishi cha SAGCOT (GRG) kilichofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bw. Jabiri Makame, na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Bw. Geophrey Kirenga.Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Mitawi (kushoto) akielezwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bw. Jabiri Makame, (kulia) namna wilaya yake inavyotekeleza kilimo biashara kinachozingatia uhifadhi wa mazingira wakati wa kikao cha mwaka cha Kikundi kazi cha Kilimo endelevu na jumuishi cha SAGCOT (GRG) kilichofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Bw. Geophrey Kirenga.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kikundi
cha Kilimo endelevu na Jumuishi cha SAGCOT (GRG) kimewakutanisha wadau
wake kujadili changamoto na kuainisha fursa zitakazo msaidia
mkulima kufanya kilimo chenye tija kinachozingatia uhifadhi wa
mazingira katika kongani ya Kilombero.
Akizungumza
kwenye kikao cha mwaka kilicho wakutanisha wadau kutoka serikalini,
Sekta binafsi, asasi za kiraia, taasisi za kifedha na watafiti
mbalimbali jijini Dar es Salaam mwishoni mwa, Naibu Katibu Mkuu
(Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Mitawi alisema lengo la
kikao hiko ni kutathmini na kupitia maazimio ya kikao kilichopita na
kuja na maboresho yatakayosaidia sekta hiyo kuleta tija kwa mkulima na
kuchangia katika pato la taifa.
“
Wakati Dunia ikikabiliwa na mgogoro wa mabadiliko ya tabia ya nchi na
kusabisha uwepo wa mvua wastani hivyo kuna kila sababu ya kuangalia
namna bora yaufanyaji kilimo ambacho ni rafiki wa mazingira na
tumekutana kukumbushana wajibu wetu tukiwa kama viongozi katika
kuhakikisha kilimo kinakuwa rafiki kwa mazingira,*alisema Bw. Mitawi.
Alisema
kilimo kinachangia kati ya asilimia 10 hadi 14 ya hewa ukaa
inayosababisha mabadiliko ya tabia nchi, na wanaoathirika zaidi na
athari za mabadiliko hayo ni wakulima ambao
hutegemea kilimo kwa asilimia 100 hivyo kunakila sababu ya maafisa
kilimo kwa kushirikiana na wadau kuhakikisha wakulima wanapata elimu
sahihi za kufanya kilimo biashara kinachozingatia uhifadhi wa
mazingira nafaida.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bw. Jabiri Makame alisema katika
wilaya yake zaidi ya asilimia 95 ya wananchi wanajiusisha na kilimo
hivyo kunakila sababu ya kuhakikisha kilimo kinachofanywa kinatunza na
kuhifadhi mazingira sambamba na kuzingatia kanuni za biashara endelevu.
“Katika
kusukuma ajenda ya kuendeleza Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa
kuzingatia uhifadhi na utunzaji wa mazingira, tumekuwa tukifanya kazi
kwa karibu na wadau wakiwemo SAGCOT ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa
kutuweka pamoja wadau kujadiliana changamoto na kuibua fursa
zinazochagiza ukuwaji wa pato la taifa sambamba na kuleta mageuzi
makubwa kwenye sekta hizo," alisema Bw. Makame.
Naye
Meneja wa SAGCOT Kongani ya Kilombero, Bw. John Banga alisema jukwaa
hilo linalosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais linafanya kazi kama
chombo cha ushauri kwa SAGCOT katika ngazi za taifa na kongani
likingilenga kuratibu na kufuatilia masuala ya kimazingira katika
programu zilizoko kwenye Ubia.
"Miongoni
mwa vipaumbele vyetu vilivyotokana na kusaini randama ya makubaliano
viliangazia ufugaji wa kisasa , kuainisha mazao ya kipaumbele ambayo
yatatoa fursa za uchumi kwa wakulima hasa wananchi wa mkoa wa Morogoro
sambamba na utunzaji na uhifadhi wa mazingira, *alisema Bw. Banga .
Alisema
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
imejipambanua zaidi katika kuhakikisha vijana wanakuwa muhimili wa
kukuza uchumi kwa kuzalisha kwa tija.
"
Azma ya Serikali inaonekana wazi kupitia programu za mafunzo atamizi,
maarufu kama Building a Better Tommorow (BBT) kwa upande wa sekta ya
Kilimo na BBT- LIFE kwa upande wa sekta ya Mifugo, hivyo kupitia
programu hizo zitakenda kuchochea na kuibua ubunifu kwa vijana kushiriki
katika kilimo na ufugaji wenye tija pamoja na kuwainua kiuchumi,"
alisema Bw. Banga.
No comments:
Post a Comment