HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 25, 2024

NHIF;Tumejipanga kuwahudumia

Na Mwandishi Wetu

 
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani kufika na kupata huduma za kujisajili na elimu ya manufaa ya bima ya afya katika Maonesho ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi(OSHA).

 
Rai hiyo ilitolewa jana na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NHIF, Catherine Kameka katika maonesho hayo  yanaendelea katika viunga vya General Tyre jijini Arusha.


“Mfuko unadhamiria kuwafikia wananchi katika maeneo yao na kutumia fursa kama hizi za maonesho, tunatoa huduma za kusajili wanachama,  kupokea maoni kuhusu huduma tunazotoa, kurejesha kadi zilizopotea na kutatua changamoto wanazokuja nazo wanachama wetu, kwa hiyo tunawaomba waje tuwahudumie," alisema Kameka.
Maonesho haya ambayo ni sehemu ya maandalizi kuelekea Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani yalianza leo na yanatarajiwa kumalizika Aprili 30, mwaka huu.

 
Akizungumzia huduma, alisema kuwa Mfuko umejipanga vyema katika kuwahudumia wanachama wake kupitia mtandao mpana wa vituo vya kutolea huduma vilivyosajiliwa na Mfuko.

 
"Tumefanya maboresho makubwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Mifumo ya utambuzi wa wanachama wanapokuwa vituoni, huduma zikiwemo za Kibingwa na bobezi lakini pia kusogeza huduma karibu na wananchi" alisema Kameka.

No comments:

Post a Comment

Pages