HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 25, 2024

YANGA WAKUBALI YAISHE KWA JKT TANZANIA

Na John Marwa 


Baada ya kutoka suluhu dhidi ya wenyeji wao JKT Tanzania, Mabingwa watetezi Yanga SC kupitia kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano Ally Kamwe amesema wanawaachia mamlaka wao ni mbele kwa mbele.


Hayo yamejiri baada ya dakika 90 za mtanange wa Ligi kuu soka Tanzania NBC PL kutamatika kwa timu zote mbili kutoka patupu na kugawana alama moja kila mmoja.
Ally Kamwe amesema hawajarudi nyuma hata hatua moja hivyo malengo yao ni kuangalia michezo iliyo mbele yao na kutetea ubingwa msimu huu.


"Ubora wa 'pitch' tunawaachia mamlaka, hatujarudi nyuma hata hatua moja, tunaenda kujipanga kwenye hesabu zetu za kutetea ubingwa, dakika 90 sidhani kama zinachambulika".


Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika juzi ilishindikana na kuahirishwa na Kamishina wa mchezo, Kamwanga Tambwe kwa sababu ya hali ya uwanja huo kujaa maji sehemu ya kuchezea kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.


JKT imeendeleza mwenendo mbovu wa matokeo msimu huu ambapo imefikisha michezo 14 mfululizo ya Ligi Kuu Bara bila ya ushindi tangu mara ya mwisho ilipoifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1.


Wananchi wamefikisha pointi 59, katika michezo 22 iliyocheza hivyo kuhitaji pointi 15 tu ili kufikisha 74 na kutwaa ubingwa wake wa tatu mfululizo na wa 30 wa Ligi Kuu Bara kwa sababu hazitaweza kufikiwa na timu yoyote.


Kwa upande wa Maafande wa JKT, katika michezo yao 23 waliyocheza ya Ligi Kuu Bara hadi sasa wameshinda minne tu, sare 11 na kupoteza minane ikiwa nafasi ya 13 na pointi 23.

No comments:

Post a Comment

Pages