Katika
kinachoonekana kuwa ni juhudi za kuhakikisha Mashirika na Taasisi za
Umma zinafanyakazi na kutoa tija chanya, Ofisi ya Msajili wa Hazina
(OTR) inayosimamia taasisi na mashirika hayo, imekuja na mpango mkakati
wa mashirika yanayoimarika kiuchumi yaanze kuwekeza nje ya Tanzania.
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. |
Bila
shaka Ofisi ya Msajili wa Hazina chini ya Msajili wa Hazina Nehemiah
Mchechu, imekuja na mkakati huo kwa lengo la kuhakikisha yale taasisi na
mashirika yanayochechemea yachechemke na yanayoinuka kiuchumi yaimarike
zaidi, hivyo kuchangia vilivyo uchumi wa Taifa.
Taarifa
zinaonyesha hadi sasa Msajili wa Hazina anasimamia mashirika 248 ya
Umma, kati yake 81 yakiwa ya biashara na 167 yasiyo ya kibiashara,
huku serikali ikiwa na hisa 56, za ndani 46 na za nje kumi (10) na
yaliyobinafsishwa 341.
Pamoja na jitihada kubwa anazoonekana
kufanya Msajili wa Hazina, mwaka huu (2024) kati ya mashirika 304, ni
mashirika 145 yaliyotoa gawio kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali, ambalo
lilikuwa Sh. Bilioni 637 wakati 159 hayakutoa kabisa.
Mwaka huu
(2024) kuna ongezeko la mashirika yaliyotoa gawio, ambapo jumla ya
mashirika 109 yaliyotoa gawio, na hivyo kufanya ongezeko la mashirika 36
yaliyotoa gawio hilo mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana 2023.
Licha
ya ongezeko hilo, Mchechu anasisitiza kuwa bado kiwango hicho siyo cha
kuridhisha, ni hali mbaya. Na anaposema ni hali mbaya bila shaka
anamaanisha bado maboresho yanahitajika, maana inafikirisha sana,
Inakuwaje iwe kati ya mashirika 304, mashirika 248 ambayo Serikali ina
hisa nyingi yatoe gawio kidogo wakati mashirika 56 ambayo ina hisa
chache ndiyo yaongoze kutoa gawio kubwa!
Kwa kauli ya Mchechu,
taswira hiyo ni somo ambalo Serikali ina kila sababu ya kujifunza namna
taasisi zake zinavyoendeshwa, kwa sababu uwekezaji wa Serikali katika
kampuni na mashirika hayo ni Sh. 3 trilioni. Kwa jumla, Serikali
imewekeza Sh. 76 trilioni kwenye mashirika na taasisi mbalimbali.
Kwa
mujibu wa Mchechu, mwaka 2019/2020, 2020/2021 na 2021/2022 Mashirika ya
Umma yalichangia Sh. 255 Bilioni, Sh. 161 Bilioni na Sh. 207 bilioni,
mtawalia, huku Kampuni na Mashirika ambayo Serikali ina hisa chache
yakichangia gawio dogo la Sh. 44 bilioni, Sh. 147 bilioni na Sh. 10
Bilioni mtawalia.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo |
Lakini anasema, kwa miaka miwili 2022/2023 na
2023/2024 Gawio kwa mashirika ya umma yanayofanya biashara lilikuwa Sh.
109 bilioni na Sh. 110 bilioni mtawalia; huku ambako Serikali ina hisa
chache yakichangia Sh. 219 bilioni na Shs. 168 bilioni kwa kipindi
hicho.
Sasa kutokana na kinachoonekana kwamba sehemu ya sababu ya
kutofanya vizuri kwa Mashirika na taasisi kadhaa pengine ni
kutojitambua kuwa wana wajibu wa kufanyakazi zinazolipa kulingana na
uwekezaji wa matrilioni ya fedha uliofanywa na serikali, kutozingatia
sawasawa kwamba mashirika hasa yale ya kibiashara yanatakiwa yawe na
ubunifu ili kuwa na sura ya kibiashara kwelikweli.
Bila shaka ni
sababu hizo na nyininezo ndizo zinaonekana zimemsukuma Msajili wa Hazina
kuibua mkakati mahsusi wa mashiri yale yenye hali njema kiuchumi yaaze
kuwekeza nje ya Tanzania ili uwe msukumo kwa taasisi na mashirika yote
ya umma kupambana kuelekea kuwekeza nje ya Tanzania.
Hata hivyo,
kuibua mkakati huo na kuzipa taasisi na mashirika kuukabili haitoshi, ni
lazima itengenezwe mbinu itakayosaidia kuzifanya mkakati huo uingine
vichwani na kuona kuwa hakuna namna nyingine mbadala itakayovusha kutoka
kwenye kudumaa kwenda kunakotaakiwa.
Bila shaka kwa kutambua
hilo, ndiyo maana Msajili wa Hazina amepanga jukwaa la Kikaokazi (CEO
Forum) cha Wenyeviti wa Bodi, Watendaji Wakuu wa Taaasisi, Mashirika ya
Umma na Wakala za Serikali, ili 'wajifungie' ukumbini na kutoka wakiwa
wmeiva juu ya kile serikali inachokitaka wakifanye.
Kwa mujibu wa
Mchechu Kiikaokazi hicho kitaperuzi kw kina maeneo muhimu ya
kufanyiakazi kutokana na maazimio yaliyojiri katika kikao kazi cha
kwanza kama hicho cha CEO Forum kilichofanyika mwaka jana (2023).
Akizungumza
na Wahariri, Julai 15, 2024 jijini Dar es Salaam, Mchechu alisema
kikaokazi hicho kitafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
(AICC) mwezi huu wa Agosti 2024, kikikutanisha wajumbe (Watendaji Wakuu
wa Taaasisi, Mashirika ya Umma na Wenyeviti wa Bodi) zaidi ya 600.
Wakati
huo, Mchechu alisema tarehe ya kufanyika kikaokazi hicho ingetangazwa
baadaye na sasa tarehe hiyo imekwishatangazwa ikiwemo kwenye Tovuti
rasmi ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, kwamba kitafanyika kuanzia tarehe
27 hadi 30 Agosti, 2024 na kitafunguliwa kwa kishindo na Rais Dk. Samia
Suluhu Hassan.
Bila shaka kikaokazi kimepewa umuhimu wa
kufunguliwa na Rais mwenyewe ili akutane uso ka uso tena na Wenyeviti wa
Bodi, Watendaji Wakuu wa Taaasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za
Serikali ili awe na wasaa mwingine mzuri wa kuwashikisha vilivyo nira
yake juu ya anavyotaka uendeshaji wenye tija wa Tasisi na mashirika ya
umma.
Siwezi kukisia, lakini hapana shaka Mheshimiwa Rais
atawafunda kwa kina wajumbe hadi wajue na kushika vilivyo dhima iliyopo
mbele yao juu ya taasisi na mashirika wanayosimamia, na pia kuwawekea
wazi tena muktadha na faida ambayo taifa litavuna kupitia taasisi na
mashirika kuitia kuwekeza nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Mchechu,
Serikali imedhamiria taasisi na mashirika ya umma kuwekeza nje ya
Tanzania kwa sababu hatua hiyo itaongeza wingo wa Taasisi hizo kukua
kiuchumi hivyo kukuza pato la taifa kwa uhakika na kwa uendelevu sanjari
na kuifanya Tanzania kushiriki vilivyo katika Diplomasia ya Uchumi.
Mashirika
ambayo kwa sasa yana sifa ya kuwekeza nje ya Tanzania Mchechu anayataja
kuwa ni yale ambayo mazingira yake ya kiutendaji yanaruhusu kama
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na Shirika la Reli Tanzania (TRC), huku
akitaja sifa za Taasisi kuwa ni uwezo wake kukua kiuchumi kama Benki za
NMB, CRDB na TCB.
Mchechu anasema, wakati Serikali ikiwa katika
mikakati ya mashirika na taasisi zake kuwekeza nje ya nchi, pia
inaendelea kufanya maboresho ya kimsingi kuhakikisha umadhubuti wa
kutosha unakuwepo katika mashirika na taasisi zote.
Katika
kuboresha na kuimarisha, kwa mujibu wa Mchechu hatua mbalimbali
zinaendelea kufanyika ikiwemo kuhakikisha Wakuu wa Taasisi na Mashirika
wanakuwa wenye uwezo unaokidhi, na katika kufanya hivyo wakuu
watakaoonekana hawakidhi wataondolewa, sanjali na hivyo, taasisi na
mashirika yatapewa uwanja mpana wa kujisimamia katika uendeshaji, badala
ya kusimamiwa na serikali.
“Katika kufanya hivi, baadhi ya
mashirika au taasisi kama hazifanyi vizuri zitavunjwa na majukumu yake
kuhamishiwa kwingine na taasisi ambazo shughuli zake zinafanana
zitaunganishwa au kubadilishiwa majukumu”, anasema Mchechu.
Mchechu
anasema, katika kuhakikisha Taasisi na Mashirika ya Umma yanakomaa
kiuchumi, sasa jukumu la kuchangia mfuko wa taifa litakuwa ni la lazima
kwa kila Taasisi na Shirika na fedha za uchagiaji lazima zitokane na
mapato ya Taasisi au Kampuni husika siyo vinginevyo.
Kwa muktadha
huo maana yake ni kwamba ili taasisi au shirika liweze kumudu ulazima
huo kuchangia gawio kutoka kwenye mapato yake itakuwa lazima kuchapakazi
kwa juhudi na maarifa na kuivaa vilivyo ya Mikakati ya serikali juu ya
Taasisi na Mashirika ya Umma Kuwekeza Nje ya Tanzania, ambayo ndiyo
kaulimbiu itakayoangaza kikaokazi cha CEO Forum cha Agosti 27, 2024
jijini Arusha.
Kulingana na tafsiri ya kaulimbiu hiyo, ni kwamba
Kikao kazi hicho kitalenga kwenda kuhimiza taasisi na mashirika ya umma
kuangalia zaidi fursa za kuwekeza au kupanua wigo wa huduma nje ya
Tanzania.
Maana kwa mujibu wa Mchechu kikaokazi hicho kitajadili
fursa za kikanda na kimataifa kwa ajili ya Taasisi na Mashirika
kuwekeza nje ya nchi sanjari na kupata uzoefu wa kiutendajikazi kutoka
kwa wataalamu wa ndani na nje ya nchi katika nyanja mbalimbali za
kiuchumi.
“Uboreshahi wa mitaji ya Mashirika haya ni kupelekea
ujuzi na utendaji kazi katika ushindani, na kuweza Kubadilisha mitazamo
na kufanya Taasisi na Mashirika hayo kuwa vichocheo vya maendeleo ya
kiuchumi.
Tunatakiwa kukumbuka mambo muhimu ambayo Wenyeviti wa
Bodi na Watendaji Wakuu wanapaswa kuzingatia katika usimamizi wa
utendaji kazi ikiwemo miongozo mbalimbali ya Uendeshaji wa Mashirika ya
Umma na umuhimu wake katika kutekeleza malengo ya Serikali kwa ufanisi",
nasema Mchechu.
Mchechu anasema, kikao hicho kitaenda kutatua
changamoto zilizopo katika uendeshaji wa Taasisi na kuweza kuainisha
mikakati iliyopo, na kwamba katika kikaokazi hicho taasisi zinazofanya
vizuri katika nyanja mbalimbali za utendaji kazi zikiwemo kutengeneza
faida na kufanya mageuzi ya utendaji na hivyo kuboresha utoaji wa huduma
zitatambuliwa na kupewa tuzo.
RAIS SAMIA
Katika kuonyesha
kuwa Rais Dk. Samia ana dhamira ya kuhakikisha usimamizi wa Mashirika na
taasisi za umma unakuwa imara zaidi Juni 11, 2024 alitoa kauli 'nzito'
kwa Msajili wa Hazina Mchechu na Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof.
Kitila Mkumbo wakati akipokea Gawio la Serikali kutoka kwa Mashirika ya
Umma na Taasisi ambazo Serikali ina hisa kidogo.
“Kwenye mageuzi
haya Mchechu na Waziri wako lazima muwe 'unpopular'. Sijawahi kusikia
Waziri wa Fedha akasifiwa hata siku moja, siku zote Waziri wa Fedha
analaaniwa, kwahiyo Mchechu na wewe utalaaniwa tu hapa, na lawama
nyingine zitakuja 'personal', nyingine kikazi, lakini hii ndiyo kazi
niliyokupa, simama na ifanye,” akasema Rais Dk. Samia.
Rais
Samia, alitoa kauli hiyo wakati akirejelea takwimu zilizotolewa siku
hiyo wakati anapokea gawio la jumla ya Sh. 637,122,914,887.59
ikijumuisha gawio la Sh. 278,868,961,122.85 kutoka katika mashirika ya
biashara na michango Sh. 358,253,953,764.74 kutoka katika taasisi
nyingine, yakiwa ni makusanyo kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Mei 2024.
Kushajihisha
kauli aliyowapa Mchechu na Prof. Mkumbo Rais Dk. Samia aliweka wazi
kwamba ndiyo maana ndiyo sababu yeye binafsi anatukanwa sana mitandaoni,
lakini amejigeuza chura anajifanya hasikii na wala hatojibu bali
anachotaka yeye ni mageuzi ya kiuchumi ili kuipeleka Tanzania mbele.
Sanjari
na hilo Rais Samia akatoa mifano ya jitihada zake namna zinavyozaa
matunda, huku Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambayo wengi walimbeza
na kuzua taharuki alipokaribisha uwekezaji wa Kampuni ya DP World kutoka
Dubai, ikiwa kinara katika ongezeko la gawio mwaka huu (2024).
"Wale
waliopiga kelele Mama kauza bahari, Mama kauza bandari, Mama kauza nini
- mauzo yale faida yake ni hii leo (TPA kuongeza mapato). Huu ni
mwanzo, tunatarajia mtapata faida kubwa zaidi kwa bandari zetu kubwa
zote ambazo ziko nchini," akasema Rais Dk. Samia katika hafla hiyo ya
kupokea Gawio.
Katika utoaji Gawio TPA iliongoza kundi la taasisi
zisizo za biashara lilonajumuisha Mashirika ambayo kwa mujibu wa Sheria
ya Msajili wa Hazina na Sheria ya Mashirika ya Umma zinawajibika kutoa
michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi baada ya kutoa gawio la Sh.
bilioni 153.9.
TPA iliifuatiwa kwa mbali mno na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyotoa Sh. bilioni 34.7, Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS) iliyotoa Sh. bilioni 21.3, Wakala wa Huduma za
Meli (TASAC) iliyotoa Sh. bilioni 19.1, na Wakala wa Usajili wa Biashara
na Leseni (BRELA) uliotoa Sh. bilioni 18.9.
Kwa kundi la taasisi
za kibiashara linalojumuisha Mashirika na Kampuni ambazo kwa mujibu wa
Sheria ya Mashirika ya Umma na Sheria ya Makampuni, zinawajibika kutoa
gawio kwa wanahisa, Benki ya NMB ndiyo iliyoongoza kwa kutoa Sh. bilioni
54.5, ikifuatiwa na Twiga Minerals (ya ubia baina ya Serikali na
Barrick Gold) iliyotoa Sh. bilioni 53.4, Airtel Tanzania (Sh. bilioni
40.8), Puma Energy (Sh. bilioni 12.2), na Kiwanda cha Sukari cha TPC
Moshi kilichotoa Sh. bilioni 10.2.
Licha ya kumkabidhi Msajili wa
Hazina kuhakikisha anayasimamia Mashirika ya Umma na Taasisi kuleta
mabadiliko chanya, Rais Dk. Samia alionya wale ambao watathubutu kumkera
kwa kumkanyagia uchumi wake anaoupambania, akisema; “Anayetaka kunikera
anikanyagie uchumi wangu. Kwenye mageuzi haya wapo wengi
watakaokanyagwa na kupiga kelele nyingi, lakini msikate tamaa, kachapeni
kazi,”
Katika muktadha huo Rais Dk. Samia akasisitiza,
ataendelea kusimamia mageuzi katika uendeshaji wa Mashirika ya Umma ili
kuyawezesha kujiendesha kibiashara na kwa tija zaidi kwa manufaa ya
Watanzania na Jukumu hili la usimamizi liko chini ya Msajili wa Hazina
na akayasihi mashirika ya Serikali kujiangalia upya katika utendaji kazi
wao ili waweze kutoa gawio kwa Serikali.
Ni wazi kwamba,
upokeaji gawio ni ishara kuwa mazingira yaliyowekwa na Serikali ya Awamu
ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia yanafanya kazi na kuwezesha
kupatikana kwa fursa ya kufanya bishara na kupata faida.
Miongoni
mwa mazingira ni kuwekwa wazi majukumu ya Msajili wa hazina kishria
ikiwemo kwamba analo jukumu kisheria katika kusimamia mageuzi kwenye
mashirika ya umma.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 8(f) cha Sheria ya
Mamlaka na Majukumu ya Msajili wa Hazina SURA 370, ikisomwa pamoja na
Kifungu cha 11(3) cha Sheria ya Fedha za Umma SURA 348 vimeweka wajibu
kwa Wakala wa Serikali, Mashirika na Taasisi za Umma kuchangia asilimia
15 ya mapato ghafi katika Mfuko Mkuu wa Serikali.
Pia, kifungu
cha 7 cha Sheria ya Mashirika ya Umma SURA 257, pamoja na mambo mengine,
kimeelekeza Mashirika ya Umma kujiendesha kwa misingi thabiti ya
kibiashara na kupata rejesho la mtaji lisilopungua asilimia 5, na
kuchangia katika Mfuko Mkuu wa Serikali.
Halikadhalika, Sheria ya
Mamlaka na Majukumu ya Msajili wa Hazina, kifungu cha 10(2)(i) kinatoa
wajibu kwa Msajili wa Hazina kufuatilia na kuhakikisha michango na gawio
kutoka katika Mashirika ya Umma inalipwa kwa wakati.
Na kifungu
cha 10A(1) cha Sheria ya Mamlaka na Majukumu ya Msajili wa Hazina
kimeweka masharti ya mashirika ya umma kupunguza matumizi ambapo
mashirika hayo yanatakiwa kutumia siyo zaidi ya asilimia 60 ya mapato
baada ya kutoa gharama ya mishahara na bakaa inayopatikana baada ya
matumizi hayo kuwekwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali.
HALI MBAYA YA GAWIO
Nikirejea
nilivyoandika mwanzo, pamoja na jitihada kubwa anazofanya Msajili wa
Hazina, ukweli ni kwamba bado hali siyo nzuri kwa Mashirika na Taasisi
za Umma kwa sababu Mchechu anasema, mwaka huu (2024) kati ya mashirika
304, ni mashirika 145 tu yaliyotoa gawio la Sh. bilioni 637 kwenye Mfuko
Mkuu wa Serikali ilhali mashirika 159 hayakutoa kitu kabisa.
Japokuwa
mwaka huu (2024) kuna ongezeko kidogo la mashirika yaliyotoa gawio,
ikilinganishwa na mwaka mwaka jana 2023 ambapo jumla ya mashirika 109
ndiyo yaliyotoa gawio, na hivyo mwaka huu kuwa ongezeko la mashirika 36,
Mchechu anasisitiza kuwa bado ni hali hiyo haitoshi kuridhisha, ni
mbaya.
Miongoni mwa jambo la kutafakari na kufanyiwa kazi kubwa
na Msajili wa Hazina kwa kunoa zaidi rungu lake la kusimamia maboresho
kwenye Mashirika ya Umma, ni kwamba wakati katika mashirika 304,
mashirika 248 ambayo Serikali ina hisa nyingi yanatoa hisa chache wakati
mashirika 56 ambayo Serikali ina hisa chache ndiyo yaliyoongoza kwa
kutoa gawio kubwa!
Mchechu anasema taswira hiyo ni somo ambalo
Serikali ina kila sababu ya kujifunza namna taasisi zake zinavyoendeshwa
kwa sababu uwekezaji wa Serikali katika kampuni na mashirika hayo ni
Sh. 3 trilioni. Kwa ujumla, Serikali imewekeza Sh. 76 trilioni kwenye
mashirika na taasisi mbalimbali.
Anasema, mwaka 2019/2020,
2020/2021 na 2021/2022 Mashirika ya Umma yalichangia Sh. 255 bilioni,
Sh. 161 bilioni na Sh. 207 bilioni, mtawalia, huku Kampuni na Mashirika
ambayo Serikali ina hisa chache yakichangia gawio dogo la Sh. 44
bilioni, Sh. 147 bilioni na Sh. 10 bilioni mtawalia.Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu
Lakini
anasema, kwa miaka miwili 2022/2023 na 2023/2024 Gawio kwa mashirika ya
umma yanayofanya biashara lilikuwa Sh. 109 bilioni na Sh. 110 bilioni
mtawalia; huku ambako Serikali ina hisa chache yakichangia Sh. 219
bilioni na Shs. 168 bilioni kwa kipindi hicho.
“Matokeo haya
kwetu yanaleta fikra mchanganyiko, ni habari njema kwa kuwa inaonyesha
uwezeshaji unaofanywa na Serikali kuendeleza mazingira wezeshi ya
biashara, kampuni binafsi inapofanya kazi na kupata faida, mazingira ni
mema,” anasema Mchechu.
Anasema, faida katika biashara ya sekta
binafsi ni kipimajoto cha mafanikio ya Serikali kuboresha mazingira ya
biashara na sera za kiuchumi huku akiwataka viongozi waliochaguliwa
kuongoza mashirika ya umma kufanya vizuri zaidi kwa faida ya Taifa na
wananchi.
“Kama tutazingatia Sh. 850 bilioni mwaka hadi mwaka
inawezekana tukawa na furaha, lakini kama tutaangalia kiwango hiki
tunachotoa sasa kwa malengo tuliyopatiwa tukiwa Arusha ya mapato yasiyo
ya kikodi yafikie asilimia 10 ya kikodi tuko mbali sana, mwaka jana
tulikuwa asilimia tatu na mwaka huu tupo asilimia tatu,” akasema.
Mchechu
anasema ni lazima ukuaji uwe wa wastani wa asilimia kati ya 60 hadi 70
ili kufikia malengo ya mapato yasiyo ya kikodi kwa asilimia 10.
“Hali
si nzuri kwa sababu bado hatuendani na kasi na maono ya Rais Samia
Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo kwa kasi nchini, maendeleo yote
yanategemea fedha, chanzo cha fedha ni vitu vitatu, Serikali kukopa,
kukusanya kodi au kupata mapato yasiyo ya kikodi. Asilimia 90 ya mapato
yasiyo ya kikodi hupatikana kupitia gawio,” anasema.
Akieleza
baadhi ya mafanikio ambayo Ofisi ya Msajili wa Hazina imeyapata Mchechu
anasema, imeendelea kushawishi kufanyika kwa mabadiliko katika sheria
yake ili kuanzishwa kwa Mamlaka ya Uwekezaji wa Umma, muswada ambao
ulipelekwa Bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza Novemba 10, 2023.
“Ni
wazi kuwa tunahitaji sheria inayojitosheleza itakayoweza kusaidia
kuleta tija katika uwekezaji mkubwa wa zaidi ya Shs. 76 trilioni
uliofanywa na Serikali kwa niaba ya Umma wa Watanzania,” akasema
Mchechu.
Mchechu anasema, katika kuimarisha utawala bora na tija
ya mashirika ya umma, Ofisi ya Msajili imezindua na kuanza kutumia mfumo
wa kidijitali wa kufanya tathmini ya bodi hali ambayo imewezesha
kukamlisha tathmini kwa wakati na kwa mawanda tarajiwa.
Anasema,
Ofisi imeanza kutumia vigezo vipya vya uendeshaji wa mashirika (Key
Performance Indicators) vilivyoingiwa kwa njia ya mikataba baina ya
wenyeviti wa Bodi na Msajili wa Hazina, vigezo ambavyo vimeboreshwa
zaidi na vimezingatia mgawanyo wa kisekta na majukumu ya msingi ya
taasisi.
“Tupo katika hatua za mwisho za kuwa na mfumo thabiti wa
kuripoti (dashboard) taarifa za kiutendaji za wakuu wa taasisi kwa
wakati na za kuaminika ili kuwezesha kufanyika maamuzi sahihi kwa wakati
(informed decision making) kwa mamlaka za uteuzi.
Ofisi pia
imefanikiwa kupitia mikataba mbalimbali ya kibiashara na pia kufanya
mazungumzo na wabia wetu kwenye sekta nyeti za uchumi; kwenye sekta ya
madini kumekuwa na mzungumzo mbalimbali tukishirikiana na Wizara ya
Madini na tumeweza kuongeza hisa za serikali katika baadhi ya kampuni,
mathalani, tumeongeza hisa za serikali katika kampuni ya madini ya Sotta
kutoka 16% hadi 20%, jambo litasaidia sana katika majadiliano ya
mikataba mingine ambayo tupo katika mazungumzo.
Pia tumekamilisha
majadiliano na kuingia mikataba mipya ya wanahisa na makampuni kama
NMB, NBC na MCCL kati ya mikataba mingi inayofanyiwa kazi, na kampuni ya
MCCL imeweza hatimaye kupata faida mwaka huu na kutoa Gawio kwa
wanahisa mwaka huu baada ya kipindi cha miaka 10,” akafafanua Mchechu.
PROF MKUMBO.
Katika
hafla hiyo ya utoaji Gawio, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na
Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, naye alisema miongoni mwa mambo
wanayosimamia ni mchango wa taasisi kwenye uchumi kuhakikisha
unaongezeka na kupunguza mzigo kwa Serikali unaotokana na kuhudumia
taasisi hizo.
“Hapa Rais ni pagumu pia kwa sababu ulituelekeza
tufanye tathmini ya mashirika ya umma ili yale ambayo yamepitwa na
wakati tukushauri uyafute na mengine tuyaunganishe, tumefanya kazi hiyo
kwa awamu ya kwanza tunaenda kuunganisha mashirika 16 na mengine manne
yanaenda kufutwa,” akasema Prof. Mkumbo.
Prof, Mkumbo akasema,
hilo ni gumu kwa kuwa alinyooshewa vidole kuwa anakwenda kuua mashirika
ya umma, lakini akasisitiza kuwa, mashirika yatakayounganishwa,
wenyeviti wa bodi ama mmoja atabaki au wote wataondoka na haiwezekani
wote wawili wafanye kazi.
“Mashirika hayo ndiyo yanafanya kazi na
mashirika binafsi, hivyo kuwa na mashirika ambayo hayaangalii biashara
vizuri, mazingira ya biashara yatakuwa magumu,” akasema.
Katika
kuwapa shime, Rais Dk. Samia aliwataka wachape kazi na akahimiza
viongozi wa mashirika, wakiwemo wenyeviti na wakurugenzi wa Bodi,
kusimamia mashirika ili mwakani zipatikane fedha nyingi zaidi.
Akasema,
licha ya mashirika mengi kutopeleka gawio serikalini, kuna mageuzi
ambayo yanafanyika huko na akawaagiza Wenyeviti wa Bodi kuyasimamia
mashirika hayo.
Akarudia onyo lake kwa viongozi wa Wizara wenye
mashirika, kwamba waache kuagiza fedha kutoka kwenye mashirika hayo na
kuwataka wawe wabunifu kuangalia vyanzo vya fedha ili wakuze mashirika
hayo.
Akawataka kufanya kazi ili kukuza mashirika yao kutokana na
serikali kuweka mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao na si kubaki
nyuma huku akisisitiza kwamba, mageuzi kwenye mashirika lazima yaendelee
ili kuendelea kukuza uchumi ambapo nchi itafanyiwa tathmini ya uchumi
wake ili kuingia uchumi wa kati.
No comments:
Post a Comment