Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA).
Hayo
yamejiri katika mkutano wa saba wa Baraza hilo uliofanyika katika Makao Makuu
ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), jijini Nairobi, Kenya
Desemba 12, 2025.
Uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 18 ya Kanuni za Utendaji za UNEP inayotaka Baraza kumchagua Rais, Makamu wa Rais pamoja na Mwandishi katika kikao cha mwisho cha mkutano wake.
Aidha, Mhandisi Masauni amependekezwa na Kundi la Nchi za Afrika,
ambalo kwa kuzingatia kanuni za mzunguko na uwakilishi wa kijiografia, limepewa
nafasi mbili za Makamu wa Rais katika Ofisi ya Baraza hilo.
Uchaguzi
wake umeidhinishwa bila kupingwa, hatua inayodhihirisha imani na heshima kubwa
ya jumuiya ya kimataifa kwa uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
masuala ya mazingira, mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu.
Kuchaguliwa kwa Waziri kushika wadhifa huo ni
heshima kubwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na unaakisi dhamira, mchango
na msimamo thabiti wa nchi katika kutekeleza sera, mikakati na ahadi za kikanda
na kimataifa kuhusu ulinzi na uhifadhi wa mazingira.
Halikadhalika, katika uchaguzi huo Waziri wa
Maji, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi wa Jamaica Mhe.Matthew Samuda
amechaguliwa kuwa Rais Baraza hilo baada ya kupendekezwa na Kundi la Nchi za
Amerika ya Kusini na Karibiani.
Pia, Vilevile,
Baraza limemchagua Balozi wa Masuala ya Mazingira na Mkuu wa Idara ya Masuala
ya Kimataifa katika Shirika la Mazingira la Uswisi Mhe. Felix Wertli kuwa
Mwandishi wa Baraza hilo. Mhe. Wertli amependekezwa na Kundi la Nchi za Ulaya
Magharibi na Nyinginezo.
Mkutano
wa saba wa UNEA uhitimishwa rasmi Desemba 12, 2025 ambapo Ofisi mpya ya Baraza
itachaguliwa kuhudumu katika kikao cha nane cha UNEA.
Mkutano
uliwakutanisha wakuu wa nchi na serikali, mawaziri wanaoshughulikia mazingira,
wataalam na wadau wa Mazingira na maendeleo endelevu kutoka nchi 193 wanachama
wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na asasi za kiraia.
Ujumbe
wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Uratibu na Wenye Ulemavu) Mhe. William Lukuvi aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi
wengine waliohudhuria nia pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja na wataalamu mbalimbali kutoka Ofisi hiyo.



No comments:
Post a Comment