NA EDITHA WILLIAM- KAGERA
WANAKIKUNDI cha wanayanga wa kijiji Rulanda kata Rulanda wilayani muleba mkoani kagera wamerudisha tabasamu kwa jamii kwa kutoa zawadi lengo likiwa ni kuendeleza umoja na mshikamano wa kikundi hicho.
zoezi hilo limefanyika tarehe 7 agost mwaka huu wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho katika kijiji rulanda likiambatana na ugawaji wa zawadi kwa watu wenye changamoto mbalimbali pamoja na maabdamano ya kukizindua rasmi kikundi hicho
Aidha baadhi ya wanafamilia waliopokea zawadi hizo wamekishukuru kikundi hicho na kuwaomba kuendelea kuwa na moyo huo wa utoaji pale watu wanapopata changamoto mbalimbali.
kikundi hicho pia kimekuwa kikishiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo lengo likiwa ni kuhakikisha jamii inasonga mbele
Aidha wamesema zoezi hilo la kuwafariji watu wenye changamoto mbalimbali katika jamii ni endelevu na umekuwa utaratibu wa kikundi hicho kufanya hivyo tangu kuanzishwa kwake,
kikundi cha wanayanga rulanda kilianzishwa tarehe 20/9/2025 kikiwa na idadai ya wanachama 78 hadi kufikia sasa kimefikisha wanachama 185
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katibu wa kikundi cha wanayanga rulanda Medison Modest amesema kuwa pamoja na mafanikio kikundi kina changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ofisi ya kudumu ya uongozi, usafiri kwa wanachama, pamoja ukosefu wa eneo maalumu ya kufanyia matukio mbali mbali.
Akijibu risala hiyo masoud ibrahimu masoud ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa risala hiyo imepokelewa na baadhi ya changamoto zilizoainishwa zitafanyiwa kazi ili kuhakikisha kikundi hicho kinasonga mbele.





No comments:
Post a Comment