HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 01, 2013

CHELSEA YAICHAPA MAN UNITED 1-0 NA KUING'OA KOMBE LA FA

 Assalaam Alaikum: Wachezaji wa Chelsea na Man United wakisalimiana kabla ya kuanza mtanange wa marudiano ya Kombe la FA, ulioisha kwa Chelsea kushinda kwa bao 1-0. Katika mechi ya kwanza, Chelsea ilityoka nyuma kwa 2-0 na kupata sare ya 2-2 Old Trafford.
 Na hilo je? Baada ya sare ya 0-0 lwa dakika 45 za kwanza, Demba Ba akahiyimisha ukame wake wa mechi 10 bila kufunga bao kwa stahili!!!!
 
 Allah Akbar; Ndivyo anavyosema Demba Ba, anayesujudu kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa kumjaalia kuipatia timu yake bao muhimu.
 Maumivu: Beki wa kushoto wa Chelsea, Ashley Cole, akitoka kupata matibabu baada ya kuumia katika mechi hiyo ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London.
 Mnatisha, ila me natisha zaidi yenu: Mlinda mlango wa Chelsea, Petr Cech akiwapa mkono washambuliaji Robin van Persie na Javier Hernandez 'Chicharito' wa Man United. Walijaribu kwa kila aina ya mikwaju, lakini hakukubali kuruhusu bao.
 No Goal: Kipa wa Chelsea, Petr Cech akipaa juu kupangua mpira wa kichwa uliopigwa na Chicharito (kulia).
 Umebaaaana!!!! Chicharito akimpa mkono Cech bila kumuangalia usoni, baada ya jitihada zake langoni kutoruhusu bao kwa dakika zot 90 za mechi hiyo.
Hongera kwa ushindi: Wachezaji wa Chelsea wakikumbatiana kama ishara ya kupongezana kwa ushindi wao dhidi ya Man United. Van Persie yuleeeeee - kama hawaoni vileeeeee!!!

No comments:

Post a Comment

Pages