HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 16, 2024

3TMBVUTaNCG6G71BJjuw34rQqwAsE58cAMBteWw1zxD7

Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam imemkuta na kesi ya kujibu mfanyakazi wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi anayetuhumiwa kumjeruhi na nyundo jirani yake Deogratus Minja kwa madai kuwa alikwenda kumshitaki Serikali za Mitaa kwamba anatililisha maji machafu mbele ya nyumba yake.

Akitoa uamuzi huo leo Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Amos Rweikiza amesema mahakama baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wote imeridhika kwamba mshitakiwa ana kesi ya kujibu kwa hiyo atatakiwa kujitetea.

Hakimu Rweikiza alimueleza mshitakiwa haki zake kwamba ana haki yab kuleta mashahidi na vielelezo na pia anaweza kutoa ushahidi wako chini ya kiapo au akitaka anaweza kukaa kimya.

Baada ya hakimu kusema hayo, wakili wa mshitakiwa amedai kuwa mteja wake atajitetea chini ya kiapo na pia hatokuwa na shahidi wala vielelezo vyovyote na  atajitetea mwenyewe.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 24, mwaka huu kwa ajili ya mshitakiwa kujitetea.

Masahi anatuhumiwa Januari 11, 2023 akiwa eneo la Mbezi Msakuzi ndani ya Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam alimpiga Deogratus Minja kwa nyundo na kumsababishia kupata madhara makubwa ya mwili mwake.

Katika ushahidi wake, Minja alidai kuwa tarehe hiyo saa mbili na nusu usiku  alikuwa akipita nje ya geti la jirani yake Masahi, alimkuta kijana wa jirani huyo, baada ya kumuona alizungumza kwa kilugha kwa sauti kubwa ambae yeye hakuielewa.

"Ghafla kijana alikuja mbele yangu akanizuia nisipite, mara geti likafunguliwa akatoka Masahi akanihoji kwamba mimi ni kama nani na kwenda kumshitaki Serikali za Mitaa, sikumjibu chochote kijana wake akanipiga ngumi,"

"Nilimgeukia jirani yangu ili amuonye kijana wake, lakini na yeye aliinua shati lake akatoa nyundo akanipiga nayo kichwani baada ya kupata maumivu makali nilianza kukimbia huku nikipiga kelele za kuomba msaada,"alidai Minja.

Alidai kuwa, alianguka chini ndipo Masahi akaanza tena kumshambulia na nyundo mgongoni, maumivu yalipomzidi aligeuka, akampiga na nyundo kwenye mkono wa kulia na kwenye bega. Jirani mmoja alifungua geti na kumsaidia kwa sababu alikuwa ana kuja damu nyingi walimpeleka Hospitali ya Bochi kwa matibabu


No comments:

Post a Comment

Pages