HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 20, 2015

MSANII MEZ B AFARIKI DUNIA


Na Mwandishi Wetu

MSANII wa muziki kutoka kundi la ‘Chamber Squad’, Moses Bushagama ‘Mez B’, amefariki dunia leo asubuhi Mkoani Dodoma baada ya kusumbuliwa na Homa ya mapafu kwa muda mrefu..
Taarifa ya kifo cha Mez B zimethibitishwa na mama yake mzazi, na kwamba alikuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Mwananchi.
 
Hivi karibuni Mez B aliongea katika kipindi cha E-News cha EATV, alisema anaendelea vyema.
“Nilikuwa na tatizo la Pneumonia tokea mwezi wa 12 nikawa nipo vizuri nilivyokuja tena Dodoma hali ikabadilika ndo nipo hospitali nimelazwa nasumbuliwa na maumivu ya kichwa na shingo.
Nategemea kuruhusiwa muda wowote na sasa hivi naendelea vizuri,” alisema. 
Mez B amewahi kulazwa na kuruhusiwa mara kadhaa katika hospitali ya Dodoma na hivi karibuni alizidiwa na kulazwa mkoani humo mpaka umauti ulivyompata.
Baadhi ya nyimbo alizowahi kuimba Mez B ni pamoja na ‘Fikiria’, ‘Kama Vipi’, ‘Kikuku’, ‘Shemeji’  ‘Nimekubali’ pamoja na ‘Ghetto langu’ aliyoshirikishwa na Marehemu Albert Mangwea.

Huyu ni msanii wa pili kufariki kutoka kundi la chamber squad. Miaka miwili iliyopita kundi hilo liliomboleza kifo cha mwenzao Albert Mangwea ‘Ngwea’ huku Mez B akiwa mstari wa mbele wakati wa mazishi yake.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

No comments:

Post a Comment

Pages