HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 28, 2015

Nyambui awaaga watanzania akisononeka

 Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui (kushoto) akikabidhiwa suti ya michezo yenye bendera ya Tanzania kutoka Meneja Mauzo wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally atakazozitumia wakati akifubndisha riadha nchini Bunei barani Asia ambako amepata mkataba wa kufundisha riadha kwa miaka miwili. (Picha na Peter Mwenda).
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Isere Sports,Abbas Ally akimkabidhi zawadi ya suti Katibu Mkuu wa zanmani wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui anayekwenda kufanya kazi ya kufundisha riadha nchini Bunei, Asia.


Dar es Salaam, Tanzania

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) aliyeachia wadhifa huo, Suleiman Nyambui ameiasa Serikali kuwa ikitaka kurudisha heshima ya michezo kama zamani ni lazima irudishe vipindi vya michezo (Physical Education PE) kuanzia shule za msingi.

Nyambui ambaye amejing'atua kuendelea na madaraka yake ya Ukatibu Mkuu wa RT baada ya kuingia mkataba wa kufundisha riadha kwa kipindi cha miaka miwili nchini Brunei barani Asia, alisema Tanzania kama haitarudisha michezo katika programu zake hakutakuwa na ushindi.

Alisema Serikali ikiweka mikakati ya michezo na kutenga viwanja vyenye ubora vya kuchezea tutaendelea kuwa wasindikizaji katika michezo yote ya riadha, soka, netiboli, ngumi na mingine ambayo kila wachezaji wakishiriki hakuna ushindi unaopatikana kulinganisha na zamani ambako wao waliwika.

Nyambui alisema Tanzania imejaliwa kuwa na wachezaji wenye vipaji na baadhi ya maeneo yanayofaa kwa ajili ya kujenga viwanja na kuweka kambi za mazoezi kwa timu za taifa kama Tanga,Mbulu, Arusha, Singida, Njombe, Makambako na Mbeya ambako hali ya hewa inaruhusu wachezaji kufanya mazoezi kwa nguvu.

Alisema kutofanyika mashindano ya michezo katika ngazi za wilaya inawanyima wachezaji wengi wenye vipaji kuonesha uwezo wao wa kujituma kutumikia taifa katika michezo kwa sababu hawaonekani.

Akipokea zawadi ya suti na vifaa vya michezo vyenye bendera ya Taifa kutoka Kampuni ya Isere Sports, Nyambui alisema Serikali pia inatakiwa kuwasaidia waagizaji na wauzaji wa vifaa vya michezo wapunguziwe ushuru ili wauze vifaa hivyo kwa bei nafuu.

Nyambui aliyewahi kuwa mshauri wa ununuzi wa vifaa vya michezo wa Kampuni ya Isere alisema katika kipindi cha miaka miwili atakayokuwa nje ya Tanzania bado ataendelea kutoa ushauri kwa watanzania wa njia nzuri ya kujikwamua.

No comments:

Post a Comment

Pages