Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

Msemaji wa polisi Uganda Felix Kaweesi auawa kwa kupigwa risasi

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Felix Kaweesi (pichani), amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana.
Taarifa zinasema Bw Kaweesi ameuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa anaondoka kwake nyumbani Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.
Walinzi wake wawili walioandamana naye pia wameuawa.
Bw Kaweesi aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana.
Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake. Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.
Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mulago. BBC

No comments:

Post a Comment