Na Elizabeth John
MAANDALIZI ya pambano la kuwania ubingwa wa IBF
Afrika, kati ya bondia Francis Cheka na Mmalawi Chiotka Chimwemwe ambalo
linatarajiwa kuchezwa Desemba 26 mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Abeid Amani Karume jijini Arusha,
tayari yamekamilika.
kwa mujibu wa promota wa pambano hilo, Andrew George taratibu za mchezo huo zimekamilika kwa asilimia 90 ikiwa ni pamoja na kumtumia tiketi bondia Chimwemwe.
George alisema ameamua kulipeleka pambano hilo Arusha kwa kuwa anaamini watu wa Arusha wanapenda ngumi na siku hiyo ni siku ya sikukuu hivyo watakuja kwa wingi pamoja na familia zao kwani pambano litaanza saa nane mchana na kwamba mabondia watapimwa uzito siku ya sikukuu ya krismasi jijini Arusha.
Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 12 ambapo Chimwemwe anajigamba atampiga Cheka ndani ya ardhi ya nchi yake hivyo amewasihi Watanzania kuja kwa wingi kushuhudia kipigo anachopewa cheka na kwamba ulinzi utakuwepo wa kutosha.

“Chimwemwe ni bondia mwenye historia ya kushinda
kwa KO na hakuna mtu asiyejua historia ya Cheka, pambano hili ni la mvutano
mkubwa, naomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kushuhudia pambano hili ambalo
linawaumiza vichwa wadau wengi wa mchezo huo,” alisema George.
No comments:
Post a Comment