Na Elizabeth John
BEKI Kisiki wa Mabingwa wapya wa Soka Tanzania Bara,
Yanga, Kelvin Yondan, amefunguka kuwa uamuzi wake wa kuihama Simba msimu
uliopita, ulidhamilia kuhamisha ubingwa kuupeleka mitaa ya Twiga na Jangwani.
Beki huyo wa kutegemewa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’ ambaye usajili wake wa kutoka Simba kwenda Yanga ulizua tafrani kubwa
kwa vigogo hao wa soka ni miongoni mwa wachezaji walioisaidia simba kutwaa
ubingwa mwaka jana.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam,
Yondan alisema licha ya kuifanyia simba mambo makubwa, vitisho ambavyo alikua
akivipata kwa baadhi ya viongozi wa simba vilimfanya adhamilie kuhama simba na
ubingwa kuuhamishia yanga ndoto ambayo ameitimiza.
“Nilikua najituma na kucheza kwa bidii sana wakati nipo
Simba lakini viongozi wa timu hiyo walikua hawaridhiki na kiwango changu pamoja
na kujituma kwa kiasi kikubwa hadi kufanikiwa kutwaa ubigwa wa mwaka jana,”
alisema Yondan.
Alisema matunda ya ubingwa huo yametokana na ushirikiano
aliopo baina ya wachezaji, viongozi na
wanachama wa klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment