Mjumbe wa NEC, Lindi mjini, Mama Salma Kikwete akihutubia
mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kineng'ena Kata ya Chakonji
akiwa katika ziara ya kuwashukuru wanachama kwa kumchagua u-NEC, kukagua na
kuimarisha uhai wa Chama wilaya ya Lindi, Feb 16, 2013. (Picha na Bashir
Nkoromo)
Kina mama wa Kijiji cha Kineng'ene wakifuatilia kwa makini
hotuba ya Mama Salma alipowahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kijiji hicho, akiwa katika ziara ya kuwashukuru wanachama
kwa kumchagua u-NEC, kukagua na kuimarisha uhai wa Chama wilaya ya Lindi, Feb
16, 2013.
Mwenyekiti wa Kamati ya miradi ya Maendeleo ya Jamii ya
TASAF, katika kijiji cha Nanyenje, Bakari Kalulu (kulia) akitoa maelezo
kwa wananchi, baada ya Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete (kushoto)
kumtaka kutoa ufafanuzi kwa nini Ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata
ulihamishwa kutoka katika kijiji hicho na kupelekwa kijiji kingine cha jirani.
Alisema uamuazi huo ulifanywa ili kutoa kipaumbele zaidi kujengwa zahanati.
Mjumbe wa NEC, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia
Fatuma Mohamed ambaye ni Mama yake mdogo, alipopita katika kijiji cha Nanyanje,
akiwa katika ziara ya kuwashukuru wanachama kwa kumchagua u-NEC, kukagua na
kuimarisha uhai wa Chama wilaya ya Lindi, Feb 16, 2013. (katikati ni Hamis
Marobona, mume wa Fatuma.
Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akiwa nyumbani Fatuma
Mohammed ambaye ni Mama mdogo wake, alikoamua kumsalimia katika kijiji cha
Nanyanje, akiwa katika ziara ya kuwashukuru wanachama kwa kumchagua u-NEC,
kukagua na kuimarisha uhai wa Chama wilaya ya Lindi, Feb 16, 2013. Wapili
kushoto ni Hamis Marobona, mume wa Fatuma.
No comments:
Post a Comment