Cynthia Ponera Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris & Tours ya Tanzania akiwa katika banda la kampuni hiyo tayari kwa kazi ya kupokea wageni mbalimbali na kuongea nao masuala mbalimbali ya biashara ya utalii kulia ni Julius Alexander Mwakilishi wa Makampuni mbalimbali yanayofanya biashara ya utalii katika Jumuiya ya Ulaya,
Kampuni ya Pongo Safaris imamekuwa ikifanya vizuri katika masuala ya utalii ambapo Cynthia Ponera anasema maonyesho haya ya kimataifa utalii ya ITB yanayofanyika katika jengo la Mense Berlin jijini Barlin ni muhimu katika biashara ya utalii kwani yanaunganisha wafanyabiashara mbalimbali duniani ambao huuziana biashara ya utalii na kuingia mikataba ya biashara ya Utalii
Cynthia Ponera Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris & Tours ya Tanzania akiwa na wenzake katika maonyesho ya Utalii ya ITB yanayofanyika katika jengo la Mense Berlin jijini Berlin Ujerumani Kulia ni Felekech Hailemariam Meneja Mkuu wa kampuni ya Village Ethiopia ya nchini Ethiopia na katikati ni Julius Alexander Mwakilishi wa Makampuni mbalimbali yanayofanya biashara ya utalii katika Jumuiya ya Ulaya
No comments:
Post a Comment