HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 26, 2013

Wananchi Wamtuhumu Mwenyekiti CCM Kupora Eneo la Shule


Na Bryceson Mathias, Mvomero

WANANCHI wa Manyinga Kata ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na Diwani Kata ya Diongoya, Jonas Van Zealand, Wamemtuhumu Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Regina Mathias, wakidai amevamia na kupora eneo shule yao na kujenga nyumba yake.

Akifafanua suala hilo kwa waandishi wa habari, Kaimu Katibu wa Kamati ya kuhakiki Mipaka ya Shule hiyo, Paulo Kokolo, iliyoundwa na wananchi katika mkutano wa hadhara hivi karibuni alisema, 

“Nasikitika kuona Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Mathias anaipotosha Jamii akiongea na na vyombo vya habari kwamba, Kamati inayofuatilia Sakata la Mipaka ya Shule ni la Kisiasa wakati Kamati ilipoundwa alikuwepo na hakuipinga”.alisema Kokolo.

Kokolo ambaye ni Kiongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kijijini hapo alisema, wananchi walipoichagua Kamati, hawakuwa na mlengo wa Itikadi za Chama bali walikuwa katika Kikao cha Hadhara cha wananchi wote na kuridhishwa wawafuatilie Sakata hilo.

Mwenyekiti, Mathias, alilalama akikanusha kuwa, wanaomfanyia Mtinga Mtima Nyongo katika Sakata hilo ni Viongoza wa Chadema kijijini hapo, ni pamoja na Katibu wa Chadema, Kasua Mkude, Mwenyekiti Ramadhani Makoko, Dismas Ngeresha na Kokolo, lila wananchi hawana Shida.

Aidha Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Manyinga Salumu Hembe alikiri kuwa shule za Msingi za Manyinga ‘A’ na ‘B’ zimeporwa na kuvamiwa ambapo Vigo wakiwemo viongozi wa Vyama na Serikali, wamejenga nyumba zao pembezoni kiasi cha wananchi kuja juu za kuunda Kamati ya Uchunguzi.

Wananchi kwa upande wao wamepinga Kauli ya Mwenyekiti Mathias wakidai, wao walipochagua Kamati kwenye Mkutano wa Hadahara wa wananchi wote ili ifuatilia uvamizi na uporaji huo, hawalenga itikadi za vyama, ila waadilifu watakaotatua uporaji ardhi ya shule yao.   
 

No comments:

Post a Comment

Pages