HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 21, 2013

YAYA TOURE ATISHIA KUTIMKA MANCHESTER CITY

ABDJAN, Ivory Coast

"Kama atapewa mkataba mpya ndani ya siku tatu au nne zijazo, sawa. Kama sivyo, hatutasubiri kwa muda mrefu na tutafungua mazungumzo ya usajili na klabu tofauti. Leo ni Jumanne, hivyo namaanisha hadi Jumamosi. Tutasema ‘Ahsante. Sawa, Yaya anaweza kutimka hapa Mei.’"

KIUNGO Yaya Toure (pichani kulia) ametishia kuondoka katika klabu yake ya Manchester City kwa kuiambia: Nipeni mkataba mpya kabla ya Jumamosi, vinginevyo naondoka zangu Etihad.

Toure, Mwanasoka Bora wa Mwaka 2012 wa Afrika, amekasirishwa na usitishwaji wa mazungumzo ya mkataba mpya kwa muda wa miezi sita.

Wakala wa Toure, Dimitri Seluk, juzi usiku amekiri kuwa: “Kama atapewa mkataba mpya ndani ya siku tatu au nne zijazo, sawa. Kama sivyo, hatutasubiri kwa muda mrefu na tutafungua mazungumzo ya usajili na klabu tofauti.

“Leo ni Jumanne, hivyo namaanisha hadi Jumamosi. Tutasema ‘Ahsante. Sawa, Yaya anaweza kutimka hapa Mei.’

“Mimi sijisikii yeye kuendelea kubaki Man City. Hii si kuhusu pesa. Anataka kuondoka kwa sababu nyinginezo.

“Yeye ni mchezaji bora na mkubwa ndani ya Manchester City, lakini anajihisi kutopewa heshima stahili na wafanyakazi wa klabu. Roberto Mancini peke yake ndiye anayemheshimu Yaya.”

Toure nyota wa zamani wa Barcelona, 29, ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi klabuni Etihad yaliko makazi ya Man City, anakolipwa pauni 220,000 kwa wiki.

Lakini Seluk amesisitiza kuwa mteja wake hajahoji mkataba mpya kutokana na nia ya kupewa ongezeko la mshahara, bali mgogoro umeibuka baada ya kucheleweshwa kwa mazungumzo hayo na mbinu zinazotumika kuyaendesha.

Na Toure, ambaye kwa sasa yuko na kikosi cha Tembo wa Ivory Coast wanajiwinda na mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil, dhidi ya Gambia iitakayopigwa jijini Abidjan Jumamosi, yu tayari kutumia sheria za FIFA kutimka.

Sheria hiyo inasema kama mchezaji hajasaini mkataba mpya hadi mwishoni mwa mkataba waake wa miaka mitatu, anaweza kuondoka, ikiwa na maana kwamba anaweza kujiuza na kununuliwa popote.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Man City, Txiki Begiristain alimruhusu Toure kutimka klabuni Nou Camp yaliko makazi ya Barcelona na nyota huyo kujiunga City, wakati huo  Begiristain alipokuwa Mkurugenzi wa Michezo Barca.

Na sasa Seluk anadai mtu pekee anayeweza kubadili hali ya mambo ni mmiliki wa klabu hiyo Sheikh Mansour: “Labda yeye kama mmiliki anaweza kuzungumza na Yaya, huenda hajui chochote kinachoendelea.”

Uamuzi huo wa Toure unaweza kuwa habari chungu zaaidi kuwahi kuzisikia Mancini kama kocha, huku ikitarajiwa kuziweka vitani klabu kubwa Ulaya zikiwamo Real Madrid, Manchester United, Chelsea na PSG.

The Sun

No comments:

Post a Comment

Pages