Nguli wa muziki wa Mwambao (Taarabu) Fatma Baraka ‘Bi Kidude’,
amefariki dunia mchana wa leo nyumbani kwake Bububu Mjini Zanzibar kutokana na
kusumbuliwa na Kisukari kwa muda mrefu mpaka umauti unamkuta.
Bikidude amekuwa mwiba katika tasnia hiyo, toka akiwa mototo
mdogo na kuliwakilisha vema Taifa ndani na nchi za nje kutokana na kipaji
chake.
Akizungumzia Msiba wa mama yake Abdallha Baraka alisema,
wamejitahidi kadr wawezavyo ili kuokoa maisha ya mama yao kwa kumkimbiza mara kwa mara hospitalini ila juhudi ziligonga mwamba kwa kuwa mungu
ndiye mwenye maamuzi zaidi.
Amesema, shughuli za mazishi zinaratibiwa kuanzia leo na
kesho atazikwa katika makaburi ya Kitumba mjini humo majira ya saa 7 mchana.
Mungu amtoa na ametwaaa jina lake liimidiwe amen.
No comments:
Post a Comment