Na Bryceson Mathias, Dodoma
DAYOSISI ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dodoma, inatarajia kutumia Shilingi Milioni 346,812,656/- ili kujenga Msingi wa Ujenzi wa Ofisi ya Dayosisi hiyo kwa nguvu ya washarika..
Hayo ya yameelezwa hivi karibuni katika Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Oktoba 20-Januari 2013 kuhusu kuchangia Ujenzi wa Ofisi hiyo, iliyotolewa iliyotolewa na Kaimu Mtunza Hazina wa Dayosisi ya Dodoma Enea Njawike.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi hiyo Alikael Manase, Jumapili iliyopita alisema, Timu yake inatarajia kuanza Ujenzi mara Moja kuanzia sasa, hasa kutokana na kazi za Kuchora Ramani, Kulipia Kiwanja, Muundo wa Jengo, Kupima Udongo na Kubadilisha Umiliki wa Kiwanja umeshakamilika, kilichobaki ni kuanza Ujenzi rasmi.
Manase alisema, Kanisa limetowa Mgawanyo wa Gharama za Ujenzi wa Msingi kwa Majimbo na Idadi ya Washarika kwenye Mabano, ambapo, Jimbo la Makao Makuu ni Mil. 214,404/-, (4,054), Mpapwa Mil. 72,620,500/- (2,648),.
Majimbo mengine ni Jimbo la Wotta Mil. 31,123,140/-(3,249), Jimbo la Kondoa Mil. 27,665,000/- (664), inayojumuisha Shilingi Mil. 345,812640/- kwa jumla ya Washarika 10,615, ambapo Kanisa Kuu limepangiwa kuchangia Mil. 52,888, 000/.
Ili kufanikisha Ujenzi huo Kamati ya Ujenzi pamoja na Uongozi wa KKKT wa Dayosisi ya Dodoma akiwemo Askofu Mkuu Amoni Kinyunyu na Kaimu Askofu Samel Mshana, umependekeza kila Msharika atoe Sh. 52, 888/- na zitakukusanywa Sh. Mil. 561,353,232/-.
Aidha uelekeo wa mafanikio ya Ujenzi wa ofisi hiyo, unafuatia hatua ya Askofu wa KKKT nchini Dk. Alex Gehazi Malasusa, kuchangisha Shilingi Milioni 115, 978,940/- katika Harambee iliyofanyika Kanisa Kuu Mwaka Jana.
Miongoni mwa fedha ya Harambee hiyo, ndiyo iliyotumika katika Uchoraji wa Ramani Mil.26/-, Kulipia Kiwanja cha Shule Mil. 3.5/-, Gharama za Muundo wa Jengo Mil.15/-, Kupima Udongo (Soil Test) Mil.4.8/-, Gharama za kubadili umiliki Mil. 2,359,796/-, Gharama za kuandaa (Quality Surveyor), Mil. 2.3/- na Gharama za Benki Laki 174,600/-, Jumla Mil. 54,1245,396/-.
No comments:
Post a Comment