Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa wawekezaji wa sekta binafsi (CEO Round Table Dinner) uliofanyika juzi usiku katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana
amesema ubinafsishaji haujafanikiwa vizuri kwani tangu sera hiyo ianze nchini
kuna viwanda havifanyi kazi wala kutoa ajira kama ilivyokusudiwa na hivyo
serikali ya Chama cha Mapinduzi inahitaji wawekezaji wa sekta binafsi katika
kuboresha huduma katika reli, barabara na viwanja vya ndege.
Akizungumza jana na waandishi wa habari, pamoja na
wawekezaji wa sekta binafsi katika
mkutano ulifanyika juzi usiku katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski.
Sera ya CCM ipo wazi, tunawahitaji wawekezaji wa sekta
binafsi na tumekuwa tukiwahitaji tangu siku zote, lazima kwanza tutambue uwepo
wao ili tuweze kuwashirikisha katika sekta ya kusaidia jamii katika hhudma za
jamii
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi amezungumza na wawekezaji
wa sekta binafsi, mwezi mmoja tangu katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) naye kuzungumza na wawekezaji hao. Wakurugenzi hao hukutana
na vyama mbalimbali kujua sera zao vyama na ushirikiano wao na sekta binafsi
nchini.
No comments:
Post a Comment