HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 17, 2013

IDADI YA VIFO MLIPUKO WA BOMU ARUSHA VYAONGEZEKA

 Baadhi ya majeruhi wa mlipuko wa bomu lililotokea mwishoni mwa wiki mjini Arusha.

ARUSHA, Tanzania


IDADI ya watu waliokufa kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea mwishoni mwa wiki wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiwa katika mkutano wa kampeni za udiwani katika Kata ya Soweto mjini Arusha imefikia watatu.

Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mlongo amesema kuwa idadi hiyo imeongezeka baada ya majeruhi mmoja kufariki wakati akipata matibabu na majeruhi wengine bado wanaendelea na matibabu.


Tukio hilo limetokea wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani mkoani Arusha.


Wakati idadi ya vifo ikiongezeka hali ya majeruhi wengine si nzuri na wamekimbizwa nchini Kenya kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.


Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya MkuuSeraUratibu na BungeWilliam Lukuvi amesema kuwa mtu hatakayefanikisha kupatikana kwa aliyehusika na tukio hilo atapata zwadi ya sh. milioni 100.

Akizungumza Bungeni mjini Dodoma leo, Mh. Lukuvi amesema kuwa serikali itatoa zawadi ya sh. milioni 100 kwa mtu atakayefanikisha kupatikana kwa mtu aliyehusika katika mlipuko wa bomu katika Kata ya Soweto mjini Arusha ambapo mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani zilikuwa zikifanyika.

1 comment:

Pages