Na Mwandishi Wetu
MLEZI wa cha New Hope Family Group kilichopo Ungindoni Jimbo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam Phares Magesa ameahidi kuendelea kuwalipia ada za shule watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao wanalelewa kwenye kituo hicho.
Magesa alitoa ahadi hiyo mwisho wa wiki ambapo alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa Chuo Cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere ambao ni Wanachama wa Jumuiya ya Umoja Wamataifa (YUNA MNMA) mahafali yaliyofanyika kituo hapo.
Alisema amekuwa akisaidia watoto wa kituo hicho mara kwa mara hivyo amewataka vijana hao kuongeza juhudi zaidi katika masomo ili wasirudishe nyuma juhudi zake katika kusaidia.
Mlezi huyo wa kituo aliwataka watoto hao kuwa watulivu na kuongeza juhudi ili siku moja waweze kufikia hatua mbazo dada na kaka zao waliowatembelea wamefikia kielimu kwani ndio njia sahihi ya kujikwamua na maisha magumu.
“Nasisitiza kuwa nitaendelea kuwasaidia hawa watoto kwani ni wajibu wangu kama mwananchi ila naomba watu wengine wenye uwezo kujitokeza kama mlivyo amua leo kufanya sherehe yenu kwa kula na watoto hao kwani wanahitaji jamii tofauti nao ili kupunguza msongo wa mawazo”, alisema.
Magesa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wasomi Tanzania alitumia nafasi hiyo kuwaasa wanafunzi wanaomaliza chuo cha Mwalimu Nyerere kuwa waadilifu na wenye maadili pindi watakapopata fursa ya kufanya kazi sehemu yoyote.
Mwenyekiti huyo alisema kumekuwa na tabii ya vijana kukosa uadilifu kwa siku za karibu jambo ambalo linashusha heshima ya vijana ambao wamekuwa wakimaliza masomo katika kwa sasa.
Alisema uadilifu ndio jambo muhimu kwa kijana yoyote ambaye anahitaji kusaidia maendeleo ya nchi yake kwani kuenda kinyume kutarudisha maendeleo na kuathiri jamii moja kwa moja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa tawi la (YUNA MNMA) Fredirick Semainda ambaye ameingia madarakani hivi karibuni alisema wao kama vijana waliamua kufanya sherehe ya kuwaaga kaka na dada zao kwa kutembelea kituo hicho ili waweze kutoa mchango wao kwa watoto hao.
Alisema wao katika mikakati yao ya mwaka wamejipangia kufanya shughuli mbalimbali za kijamii hivyo hii ya kutembelea kituo hicho ni moja ya utekelezaji wa mipango yao.
Semainda alisema katika mahafali hayo ya pili tangu kuanzishwa kwa YUNA MNMA wahitimu 52 wametunikiwa vyeti jambo ambalo wanaliona kuwa ni la mafanikio makubwa.
Mwenyekiti huyo alisema wataendelea kufanya shughuli za kijamii kama hiyo waliofanya mwishoni mwa wiki ambapo walishiriki kuandaa chakula cha mchana na watoto hao na kula nao pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo mchele kilo 40, mafuta, sabuni, madaftari, kalamu na nguo mbalimbali.
Aidha alisema katika sherehe hiyo wanafunzi wanachama wa YUNA MNMA walichangisha shilingi 43,000 kwa ajili ya kuwapatia madawa watoto ambao wanaishi katika kituo hicho.
No comments:
Post a Comment