Mathis Bolly, akiwajibika dimbani akiwa na jezi namba 11 ya nahodha wa Ivory Coast Didier Drogba. Hii ilikuwa ni mechi ya ushindi wa 3-0 iliyovuna Ivory Coast dhidi ya Gambia.
Bolly akiwa katika jezi namba 35 ya klabu yake ya Fortuna Düsseldorf inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga.
Kuelekea safari ya Ivory
dhidi ya Gambia nah ii ya juzi dhidi Taifa Stars, kocha wa Ivory Coast, Sabri
Lamouchi akatangaza kumpa Bolly jezi ya namba 11 ya kikosi chake, miezi
michache tangu yoso huyo alipochagua kuichezea nchi hiyo na kuikacha ile ya Norway
alikozaliwa
KUTEMWA kikosini kwa nahodha wa kikosi cha Tembo wa Ivory
Coast kilichotua nchini kuivaa timu ya taifa ya Tanzania , kulizua maswali miongoni
mwa wadau wa soka la Afrika kuwa nani ataitwa badala yake? Nani atavalishwa
jezi yake (namba 11)?
Lakini pia je, beji ya unahodha ya Drogba atavaa nani?
Karibia maswali yote yalipata majibu kufikia jana jioni wakati Stars iliposhuka
ndani ya dimba la Taifa kuwavaa wageni wao hao Tembo wa Ivory Coast ,
naamini kila swali lilipata jibu muafaka.
Hapa tunamuangalia yoso Mathis Gazoa Kippersund Bolly
‘Mathis Bolly,’ kijana mwenye miaka 22 aliyeitwa kujaza nafasi ya Drogba
kikosini, lakini heshima yake ikasogezwa mbele zaidi kwa kuvalishwa jezi namba
11 ya kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast .
Mathias Bolly ni jina jipya katika soka la Afrika, ambaye
ukiondoa kupangwa kama nyota wa akiba juzi dhidi ya Stars, mechi pekee kwa
kinda hilo kuvaa jezi za Ivory Coast ilikuwa ya
ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Gambia ,
mechi iliyopigwa Juni 8, siku ambayo Taifa Stars ililala 2-1 dhidi ya Morocco jijini
Marrakech.
Kuelekea safari ya Ivory dhidi ya Gambia
nah ii ya juzi dhidi Taifa Stars, kocha wa Ivory
Coast , Sabri Lamouchi akatangaza kumpa Bolly jezi ya
namba 11 ya kikosi chake, miezi michache tangu yoso huyo alipochagua kuichezea
nchi hiyo na kuikacha ile ya Norway
alikozaliwa.
Uamuzi tata uliozua utetezi kwa kocha Lamouchi
Kitendo Bolly kupewa jezi ya Drogba, kilizua shaka na
wasiwasi miongoni mwa mashabiki wan chi hiyo, kwamba huenda kocha amehitimisha
rasmi zama za mkali wao huyo kikosini kwa kumtema kiaina, lakini Lamouchi
akafungua mdomo kujitetea.
Lamouchi anasema kuwa, hajafunga milango kwa Drogba, bali
alilazimika kuigawa jezi hiyo kutokana na kanuni ya Fifa inayotaka nyota 23
kikosini kugawiwa jezi kuanzia namba moja hadi 23 bila kuiruka yoyote pasipo
sababu ama idhini maalum.
“Watu hawapaswi kufikiria kwamba nimemtupa moja kwa moja nje
ya kikosi mshambuliaji Drogba,” alijitetea Lamouchi.
“Nilichofanya ni kutekeleza sheria za soka chini ya
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) na lile la kimataifa Fifa kwa kuigawa kila jezi
moja kwa kila mchezaji.
“Kuna wachezaji 23 kikosini ambao wanapaswa kuvaa kuanzia
namba 1 hadi 23 na mtu anahitaji kuivaa hiyo jezi namba 11 wakati Drogba anapokuwa
nje ya kikosi hiki kama ilivyotokea,” alifafanua Lamouchi katika mahojiano yake
na Supersport.
Kuonesha hajamtema moja kwa moja, Lamouchi amemtaka Drogba
kujiweka fiti kabla ya Agosti itakapokuwa ikijiandaa kwa mechi ya mwisho dhidi
ya Morocco ,
ili kurejea kikosini na atavaa jezi yake namba 11 ‘aliyorithishwa’ Bolly kwa
muda tu.
Mathias Bolly ni nani na ametokea wapi?
Mathis Gazoa Kippersund Bolly, ni Mu-Ivory Coast aliyezaliwa
Novemba 14, 1990 nchini Norway na kuanzia maisha ya soka la utoto katika klabu
ya vijana wadogo ya Holmlia iliyofungua milango ya kipaji chake katika idara ya
kiungo wa kati.
Mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 18, Bolly akaihama akademi
yake hiyo na kusajiliwa na mabingwa mara tano wa Ligi Kuu ya Norway, iitwayo Lillestrøm
Sportsklubb, ambayo kwa sasa inatambulika kama
Tippeligaen inayoshirikisha timu 16.
Kuanzia hapo, akawa mhimili wa kikosi cha Lillestrøm hadi mapema
mwaka huu, alipoihama klabu hiyo na kutua Fortuna Düsseldorf inayoshiriki Ligi
Kuu ya Ujerumani Bundesliga. Uhamisho huo, ukahitimisha maisha yake Lillestrøm
alikocheza mechi 60 na kufunga mabao saba.
Ni uhamisho uliombatana na uamuzi wa yoso huyo kukataa mwito
wa kuichezea timu ya taifa ya Norway
na kuchagua kuchezea Ivory Coast ,
kama kanuni na sheria za Fifa zinavyomruhusu.
Uamuzi huo ndio uliomsukuma Lamouchi kumjumuisha kikosini
ili kupigania safari ya Ivory Coast nchini Brazil zinakofanyika fainali zijazo
za Kombe la Dunia, kisha kumpa jezi ya nahodha Drogba aliyetemwa kwa sababu za
majeruhi.
Je atadumu nayo huku akimudu kuitendea haki jezi hiyo? Ni
suala la kusubiri na kungoja, lakini majibu ya awali yalipatikana kupitia
alichokionesha katika mechi ya Ivory Coast dhidi ya Gambia Juni, ingawa
alikalia benchi katika mechi dhidi ya Taifa Stars juzi.
WASIFU
JINA KAMILI: Mathis Gazoa Kippersund Bolly
KUZALIWA: Novemba 14, 1990
ALIKOZALIWA: Norway
KLABU YA SASA: Fortuna Düsseldorf
NAFASI DIMBANI: Kiungo
NAMBA YA JEZI: 35
Makala hii
imeandaliwa na Salum Mkandemba kwa msaada wa mashirika ya habari
Barua pepe: mkandemba@yahoo.com
Simu namba:
0789 947 744
No comments:
Post a Comment