Wachezaji wa timu ya wanawake ya mpira wa Peter ya Media NSSF All Stars wakikaguliwa kabla ya mpambano na tinu ya Bunge ya mpira wa Peter wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma leo
Wachezaji wa timu ya Mpira wa Pete ya Bunge wakikaguliwa kabla ya mchezo.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai akisalimiana na wachezaji wa timu ya NSSF Media All Stars kwa upande wa wanaume kabla ya mchezo kuanza dhidi ya timu ya Bunge Sports Club.
Wachezaji wa Bunge Sports Cluba na NSSF All Stars wakisikiliza mawaiza kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa mchezo huo wa kirafiki uliochezwa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. NSSF All Stars kwa upande wa Mpira wa miguu walishinda 1-0 na kufanikiwa kunyakuwa kikombe na kwa upande wa mpira wa Pete Bunge walishinda 31-10
Naibu Spika Job Ngugai (wa pili kulia), Mkurugenzi wa NSSF, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dk. Ramadhan Dau (wa pili kushoto), Mbunge Urambo Magharib, Profesa Juma Kapuya (kulia), na Mbunge wa Sunve, Richard Ndassa wakifutilia mchezo mpira wa miguu katika ya NSSF Media All Stars na Bunge Sports Club
Nahodha wa NSSF All Star upande wa mpira wa Pete akikabidhiwa Kikombe na Naibu Spika baada ya kuwa washindi wa pili
Nahodha wa Mpira wa Peter kwa timu ya Bunge, Mbunge wa Viti maalum (CUF), Mkiwa Kimwanga akiwa Kombe la ushindi baada ya kukabidhiwa na Naibu Spika Job Ndugai.
Nahodha wa timua NSSF Media All Stars kwa upande wa timu mpira wa Miguu, Majuto Omari akionyesha Kombe baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau baada ya kuifunga timu ya Bunge Sports Club 1-0.
Wachezaji wa timu ya Bunge Sports Club wakishangilia baada ya timu ya mpira wa pete kuibuka na ushindi na timu ya mpira wa miguu kuibuka mshindi wa pili
Wachezaji wa NSSF Media All Stars wakishangilia baada ya mchezo kumalizika.
Wachazaji wa NSSF Media All Stars wakicheza muziki baada ya kumalizika kwa mchezo.
No comments:
Post a Comment