HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 16, 2013

Chuki ni uchafu wa moyo, na ni hasara kuwa nayo!

 Na Bryceson Mathias

SITAKI nikose kuamini kwamba, sasa nchini kuna Maharamia wasio na utu ambao wana chuki, lakini hawajui  kuwa ni hasara kuwa navyo.
Rafiki wa chuki ni Kisasi cha kulipiza, ambapo mtu hata kama alikuzidi Elimu, Ujuzi, Akili, Maarifa, Hekima,  Busara  na kukubalika na watu, usimuwekee Nyongo kiasi cha kufikia kulipiza Kisasi ambacho bila kufahamu, matokeo yake yanaweza kuiharibu Jamii nzima!.
Cha kusikitisha, ninachokisema, hivi sasa kimekithiri nchini, ambapo tumeshuhudia wanasiasa kwa ajili ya kujipatia vyeo na Heshima za dhamana walizokabidhiwa na wananchi, wamekuwa na Chuki iliyohodhi Uchafu wa Mioyo yao bila kujua itawagharimu.
Uharamia huo, ndio ambao umesababisha hata wazazi, mfano;hivi karibuni Tabora, Mama amemuunguza kwa kumchoma na Bati la Moto mwanae wa kumzaa kwenye Miguu, kisa amekwenda kuzurura.
Tumewashudia mara kadhaa akina mama wanawachoma Moto au mateso mengine ya kinyama, wafanyakazi wa nyumbani hata ndugu waliowachukua makwao ili waishi nao, wakiwemo  wanafunzi walio Yatima, hadi inafikia wanaokolewa na Jamii (Nguvu ya Umma).
Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? 
Mimi, Bwana (Mungu), nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake”. Isema Biblia  Yeremeia 17.9-10.
Mioyo michafu, inawadanganya watanzania miongoni mwetu ili kuharibu tunu nzuri ya Amani tuliyonayo kwa Uroho wa Madaraka na Kipato kiasi cha kuwaumiza, kuwajeruhi, na kuwakatisha maisha wasio na hatia, ifahamike tutalipwa kwa njia, matunda, sawa na matendo yetu.
Hivi hatujiulizi, kwa nini uchaguzi mdogo kama wa Madiwani ufikie kupoteza Damu na Roho za watu? Tume ya uchaguzi (NEC) mlikuwa wapi kufanya kazi na makatazo ya kuwazuia viongozi wa Wilaya na mikoa kama mlivyofanya Arusha na Uchaguzi ukawa shwari?
Sasa nimeaamini, kwa nini watu wanasema vyeo vya Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa viondolewe; kumbe vinasababisha adha maana hawachaguliwi na wananchi, wanaweza kufanya wanavyotaka kwa kuwa hawana Uchungu na madhara ila mzigo wa bwana Ufike.
Sasa nakubali kwamba, kama Jeshi l Polisi na lenyewe litatii bila shuruti kuingilia kazi za wana siasa likaamua kufanya wajibu wake liliokusudiwa kufanya bila mashinikizo ya wanasiasa Uchwara na watawala, Chuki na Uchafu wa Moyo unaosababisha hasara; hautakuwepo.
Watawala; Je, Usalama mzuri na tulivu uliofanywa bila Hasira na Visasi Arusha, nai mkataba aliosainisha, Barack Obama, kama Mkopo nafuu? Kama ndivyo alivyofanya kuwatundisha Demokrasia ya kweli, hilo ni zuri liigwe! Llakini mfanye hivyo siku zote, isiwe kama Usafi Dar sasa kuchafuu!.
Kama ilivyo kwa Viongozi wa Dini ni Makamanda wa Kiroho, na Polisi Makamanda wa Mambo ya Kimwili, basi kila mmoja anatakiwa kutii sheria bila shuruti. Polisi wasiache kanisani au misitini kushambuliwe na viongozi wa Dini wauawe au kujeruhiwa bila kutupa ripoti.
Kama Polisi wanataka Viongozi wa Dini, Wananchi na Jamii kwa Ujumla Itiii Sheria bila Shuruti, basi na Polisi watii bila Shuruti kwa kutowaingilia wananchi, wanasiasa katika mambo yao.
Polisi wawe walinzi tu na watendaji wa kazi isiyo na mashinikizo, hasa pale ambapo mmoja kati yao anapozidiwa kwa hoja za Elimu, Ujuzi, Akili, Maarifa, Hekima,  Busara  na kukubalika na watu.

No comments:

Post a Comment

Pages