HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 15, 2013

Diwani wa CCM adai Waziri Makala hampendi!

Amosi Makala
Na Bryceson Mathias, Mvomero
 
DIWANI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mhonda, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Salum Mzugi, amesema, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makala, Hampendi. Kwa sababu hayumo kwenye Mtandao wa Kundi lake.
 
Diwani Mzugi alisema hayo 15.7. alipohojiwa na Gazeti iwapo anafahamu siku hiyo ni ya mwisho aliyotakiwa na Waziri Makala na Mbunge wa Mvomero, awe amerejesha Mabati 100 aliyotoa 2010 kwa ajili ya Madarasa mawili ya Shule ya Msingi Ngomeni ‘A’(Mabogo).
 
Mzugi alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku ya Tano baada ya Waziri Makala ambaye ni Mbunge wa Mvomero, kumtaka Diwani huyo awe amerejeaha Mabati hayo ambayo Mwananchi Nasibu Abdalah almaarufu (Nduli) alimtaka Waziri awaondolee utatanishi wa Bati hizo hadi sasa ahazieleweki zilipo.
 
“Mhe. Mbunge tunaomba utuondolee utatanishi wa Bati 100 ulizotoa kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa mawili ya Ngomeni, baada ya kuombwa na wananchi, ikiwezekana tuondoke mguu kwa mguu hadi kwa Diwani Mzugi, ili zichuliwe zitunzwe Ofisi ya Kijiji”.alisema Nduli.
 
Akijibu hoja hiyo Waziri Makala alisema, amechoshwa kusikia kero hiyo ikiulizwa kila mara, hivyo analimpa Diwani Mzugi siku Tano toka Julai 11-15, 2013 awe amerejesha Bati hizo ili zifanyiwe kazi iliyokusudiwa.
 
Makala ambaye alikuwa katika Ziara ya Vijiji 24 jimboni kwake, pia aliwaeleza wananchi kila Kiongozi atabeba Msalaba wake, pia akimtaka Diwani wa Sungaji, Athumani Mkimbu, naye arejesha fedha za Zahanati ya Mlaguzi iliyodanganywa iko kwenye Lenta wakati ni Msingi.
 
Aidha Mzugi alikiri kupewa Bati hizo, na kwamba Viongozi wa Kijiji na Walimu wa Shule, walimtaka azitunze ili ziongezwe nyingine Mbili, na kudai aliziweka dalini kwake, hata ukiingia mlangoni kwake zinaonekana.
 
“Nashangaa Mbunge, amekuwa hanipendi! Sielewi sababu sipo kambi yake ambayo fulani na fulani (majina yanahifadhiwa), ambapo 11.6.2013 akiwa na mkutano Kichangani, Kijana Nduli alitumiwa kuuliza swali ili kunichafua”.alisema Mzugi amabye hakuwepo siku hiyo.

Habari toka kwa baadhi ya wananchi zinadai kwamba, Diwani Mzugi alizungungumza na baadhi ya wananchi wa kitongoji kimoja, wakatae kuhamishwa kwa bati hizo, kwa madai zinapelekwa ili zikaezeka jingo la Polisi Turiani, jambo ambalo Mzugi amelipuuza.

1 comment:

  1. nakuapreciate mkuu piga vita wez katika vijiji vyetu mm nipo kunke

    ReplyDelete

Pages