HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 22, 2013

Kasi ya Chadema inanifanya nisigombee Uenyekiti CCM 2015

Na Bryceson Mathias, Kongwa

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kitongoji cha Morisheni Kata ya Mjini Magharibi wilayani Kongwa amesema, Kasi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inatisha na kumtia hofu, kumfanya asigombee tena 2015.
Mwenyekiti huyo, Joel Mbanga, alisema hayo Julai 21, mwaka huu akidai kwamba, hivi sasa si siri, Chadema kinakubarika sana na Wananchi, hivyo kama ukikurupuka kugombea kama huna sera utagalagazwa halafu Uaibike.
Akizungumza na Habari Mseto Blog, Mbanga alisema, Sumu ya Hoja na Sera zilizomwagwa na Wabunge watano waliofukuzwa bungeni na Naibu, Spika Job Ndugai, Mbunge wa Jimbo hilo, imekidhoofisha CCM.
“Sumu iliyomwagwa Kongwa na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, na Meya wa Musoma Alex Kasurura, ni heri Ndugai asingewatoa, kusisa wametuachia Makovu 2014/15 ki-chama.
Alidai pamoja na kuwa, mwenyewe anapenda kuwatumikia wananchi, na kuahidi kumchukulia fomu na kumjazia. Lakini anadai anasita, akiogopa kuaibishwa, kama ilivokuwa Arusha kwenye uchaguzi wa madiwani.
Alisema Kijiji chao kina Vitongoji 14, lakini ukifuatilia hali ya kisiasa na mwamko wa Ukombozi ulivyo katika Vitongoji vinane, inadhihirisha kuwa hali si shwari ndani ya Chama changu.
Aidha Mwenyekiti wa Chadema wilayani humo, Juma Shibiriti, amekiri kuwepo na Hamasa kubwa akisema wameikata Koo CCM, “Ni kweli Kasi ya Chadema iliyopo inawatisha Mahasimu wetu kila mahali, kijijini na Mjini”.alisema Chibiriti.

No comments:

Post a Comment

Pages