HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 23, 2013

KKKT Dodoma kutumia Mil.32.9 kumalizia Nyumba ya Askofu Ngowo

Askofu wa Dayosisi ya Dodoma Amoni Kinyunyu akiwa na Kamati ya kumalizia Nyumba ya Askofu Mstaafu Festo Ngowo.

Na Bryceson Mathias, Dodoma

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amosi Kinyunyu amesema, Kanisa linakusudia kutumia Shilingi Mil.32,868,765/- kumalizia nyumba ya Askofu Mstaafu Festo Daudi Ngowo, ambaye sasa anaumwa na  hawezi kuzungumza.

Fedha hizo ni nguvu ya Washarika wa Dayosisi hiyo, na zimegawanywa kwa Majimbo yote Manne na Dayosisi hiyo na kiasi chake kikiwa kwenye mabano.

Jimbo la Wotta lina Washarika 2,831 (Mil. 2,300,000/-), Jimbo la Mpwapwa Washarika 3,048 (Mil. 6,903,000/-), Jimbo la Kondoa Washarika 716 (Mil. 2,287,460/-) na Jimbo la Makao Makuu Washarika 5,084 (Mil. 21,377,540/-).

Viongozi wa Majimbo nao kwa upande wao, wamezigawanya fedha hizo kwa Idadi yaWasharika katika Sharika zao, na Wachungaji wa Sharika wamezigawanya kwa Idadi ywa Waumini kwenye Mitaa yao, jambo litakalorahisisha upatikanaji wa fedha na Vifaa.

Akizungumza na Kamati ya kuhamasisha uchangiaji huo mbele Kaimu Askofu Samwli Mshana, Mwenyekiti wa Kamati ujenzi na Wahamasishaji watakaopita sharikani kusimamia Harambee ya Changizo hilo, Askofu Mkuu wa KKKT Dodomaa, Amoni Kinyunyu, alisema.

“Dayosisi inakusudia kusimamisha shughuli zingine zote za machangizo ya fedha kwa ajili ya Miradi mbalimbali, ili kuhakikisha Nyumba ya Akofu Msataafu inamalizika, na ikibidi anahamia kabla ya Mwezi Septemba mwaka huu.

“Tusipomshughulia Askofu Ngowo na tukahakikisha anakaa mahali pazuri Dayosisi itakosa Baraka kwa Mungu, wakiwemo Viongozi , Waumini na kila aliyehudumiwa naye kiroho wakati akiwa na afya nzuri ya kuwahudumia kwa Neno la Mungu”. Alisema Askofu Kinyunyu.

Aliongeza kwamba, hata anapokuwa kwenye ziara za kikazi za Kanisa na kuonana na Ma-Askofu wenzake, Wachungaji, Wa-Injilisti, Wahudumu wa Ofisi wa Kanisa (Parish Workers) na Waumini, wamekuwa wakimuulisha afya ya Askofu Ngowo, na kuhoji Shughuli ya kujenga nyumba yake ya kuishi inakwendaje.

Julai 28, 2013, itakuwa ndiyo siku ya Harambe ya kuchangia ili kupatikana kwa fedha hiyo katika Dayosisi yote ya Dodoma KKKT, ambapo fedha zitakazopatikana zitakwenda moja kwa moja kwenye Ujenzi huo unaoanza mara moja.

Maeneo ya Umaliziaji wa nyumba hiyo ni Vifaa vya mfumo wa Maji, Vifaa vya mfumo wa Umeme, Utandazaji wa Nyaya za Umeme, Fremu za Milango ya Mbao, Grili za Madirisha na Milango, Vifaa vya Dari na Utengenezaji (Blundering), na kupiga ripu.

Aidha katika Shukurani kwa walioshiriki kuchangia nyumba hiyo, Msaidizi wa Askofu Mshana katika Barua Kumb. DAD/MA/2 VoL.2 ya Julai 5,2013 Umaliziaji wa Ujenzi  wa Nyumba ya Askofu Mstaafu Ngowo alisema,

“Nawaomba tena Washarika wote wa KKKT Dodoma na nje, kushiriki kwa mara nyingine kumchangia Askofu Ngowo, ili wapokee Baraka za Mungu kwa kumtunza Ngowo wakati huu ambao hasemi, maana Mnamfahamu utumishi wake uliotukuka”.

No comments:

Post a Comment

Pages