Na Bryceson Mathias
Ni Nia yangu kutaka kumfahamisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma), Celina Kombani na Wanasiasa wengine wajua kuwa, hakuna siri yoyote chini ya Jua, ila Siri zote ni za Mungu Baba.
Biblia Takatifu katika Kumbukumbu la Totari 29:29 inasema, “Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii”.
Wakati Rais Jakaya Kikwete, alimwagiza Waziri Kombani, kumwandalia, aliyekuuwa Naibu Waziri Mkuu, mstaafu, Agustino Mrema, mafao yake. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Benson Bana hajuii nafasi za Kukaimu katika Umma zinalipwa?.
Ieleweke, Rais Kikwete aliyesema akifunga kongamano la amani ya nchi kwa viongozi waandamizi wa vyama vya siasa na serikali lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia nchini (TCD).
Yakobo 3:6-8 ‘Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe’.
Binadamu anaweza kuwafuga wanyama, na amefaulu kufuga viumbe vyote--wanyama wa mwituni, ndege, nyoka na viumbe vya baharini. Lakini hakuna mtu aliyeweza kuufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu, hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua’
Nimesnukuu maandiko ya ulimi nikishangazwa na maneno ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Benson Bana aliyesema Rais kumwagiza Waziri mwenye mamlaka husika kushughulikia mafao hayo ya Mrema siyo kwamba ni tiketi ya kulipwa.
Alisema, “Waziri katika utekelezaji wake ataangalia Sheria inasema nini na kisha atamwandikia Rais kwa kumshauri kwamba agizo lako haliwezi kutekelezwa kwa sababu mbalimbali kwa kuwa cheo hicho hakikuweko katika Katiba.
“Waziri atamwandikia Rais kumjulisha kuwa mhusika hana mafao anayodai kwa kuwa alishalipwa akiwa Waziri pamoja na yale ya ubunge”.
Hivi kama Rais kamwagiza Waziri mwenye Mamlaka husika kushughulikia mafao hayo, ni kweli siyo kwamba ni tiketi ya kulipwa? Dk. Bana anataka kumfanya Rais ni mwanainchi wa kawaida au ni Mtu mwenye Mamlaka?
Dk. Bana ni Mkristo, hivi hajui maandiko haya (Mathayo 8:8-9) yanasemaje? “Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.
Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya”.alisema Akida.
Hivyo Rais Kikwete ana Mamlaka ya kumwambia Kombani, Nenda, huenda; na Njoo, huja; na Waziri wake, Fanya hivi, atafanya. Kama tunavyoona Polisi wakiambiwa na Viongozi wao Piga Mabomu wanapiga, Tawanya Mikutano wanatawanya, Mwagia Maji ya kuwasha wanafanya.
Ni rai yangu Viongozi wenye Elimu, tusiwapotoshe wananchi wakajifunza kupuuza maagizo ya Watawala na kwa amri ya Piga tuu, wakajikuta wanapigwa kiasi cha kuhatarisha maisha yao, kumbe wamepotoshwa na wasomi tunaowategemea.
“Alipotukanwa yeye hakujibu kwa tukano; alipoteseka yeye hakutoa vitisho, bali aliyaweka matumaini yake kwa Mungu, hakimu mwenye haki (1petro 2:23).
Tabia za kuzuia Haki zinazofanywa na baadhi ya viongozi, zinanikumbusha Jinsi ambavyo wananchi wanapopewa haki za kisheria na Mahakama, baadhi ya viongozi serikalini, huinuka na kukata rufaa!
0715933308
No comments:
Post a Comment