HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 29, 2013

Mhubiri Mkongo aonya watanzania wasidanganywe!


 Mhubiri Mahano Jean toka Kongo akifundisha.
 Mhubiri Mahano Jean wa Kongo akisikilizwa kwa makini.

 Na Bryceson Mathias, Dodoma
MHUBIRI wa Kimataifa wa Kongo, Mahano Jean, amewaasa na kuwaonya watanzania wasidanganywe na watu wasio na Upako wa kwa sababu hata wao ni wateule wa Mungu, na kwani ajuaye thamani yao, hivyo mtu asiwanunue kwa bei rahisi.
Akifundisha katika Semina ya Neno la Mungu kuhusu Upako Alhamsi Julai 25, Kanisa la PAC Makole Dodoma, Jeani alisema Watanzania wasidanganywe na Wahubiri Uchwara wanaojigamba watawaombea na kuwaondolea matatizo na kuwapa Utaji, akidai hao ni waongo!.
Alisema, Watanzania ni Wateule wa Mungu, wenye Upako wa Ukuhani, Ufalme, Unabii na Kukubalika kama alivyowaahidia, ambapo aliwaasa kama wakimtafuta Mungu kwa bidii na kutii maagizo yake, atathibiti hayo na kuiadhibu milango ya Adui zao.
“Wapo baadhi ya Wahubiri wanaohubiri wakijidai, nilikuona kwenye ndoto una tatizo hili na lile, kama unataka nikuombee tatizo hilo litoke na upate utajiri….njoo na dola kadhaa nitaomba na matatizo yako yataondoka na utabarikiwa.
“Nakupa Changamoto, usikubali Uongo huo, wewe ni mtu mteule wa Mungu, alikuchagua tangu ukiwa tumboni mwa Mama yako, alicho nacho hata wewe unacho kwa sababu una Upako waUkuhani, Ufalme, Unabii na Kukubalika, huna haja ya kumpa dola, Omba mwenyewe na Mungu atakupatia”
Alisema, hakuna mtu ambaye alipewa huduma na Mungu aiuze, ila Biblia inasema umepewa bure na wewe toa bure! Aliongeza kwamba, wapo watumishi wanajipaka manukato ya kuwavutia watu, wakiwatisha na kuwaogopesha kuwa usipotoa fedha huponi.. hao ni waongo!
Alikwenda mbali akionya kuwa, wengine wamekuwa wakihaha kuwahamisha watu kutoka Kanisa moja kwenda lingine wakidhani kuna utofauti, hakuna utofauti ila tatizo ni watu kutokuwa na Upako!
Aidha awali Jean alifundisha aina za Upako ambapo alizitaja kuwa ni wa Roho Mtakatifu ambapo alizitaja kuwa ni, Upako wa Mafuta, Mavazi na Upako wa Kuzaliwa nao, kama ule wa akina Samson, Elia, Samweli na wengine, ambao alisema ukiwa nao unakuwa na akili, unajua kupanga mambo, na kubaini baya na zuri.

No comments:

Post a Comment

Pages