Rais Jakaya Kikwete akiwasili katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Upanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuaga miili ya askari saba waliouawa wakati wakilinda aman nchini Sudan.
Rais Jakaya Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Davis Mwamunyange akiomuongoza Rais Kikwete wakati wa kuaga miili ya askari waliouawa Darfur.
Moja ya miili ikishushwa kwa ajili ya kuagwa kwa heshima za kijeshi.
Baadhi ya ndugu wa askari waliouawa Darfur wakiwa na huzuni.
Familia za askari waliouawa zikiwa na nyuso za huzuni wakati miili hiyo ikiwasili katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.
Askari wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Private Peter Muhiri Werema.
Majeneza yaliyokuwa na miili ya askari waliouawa Darfur.
Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa Darfur, Sudan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa Darfur, Sudan.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga miili ya askari saba wa JWTZ waliouawa Darfur wakati wakilinda amani.
Baadhi ya maofisa wa JWTZ wakitoa heshima za mwisho.
SGT. Shaib Othman
CPL. Osward Paul Chaula
CPL. Mohamed Juma Ally.
CPL. Mohamed Chukilizo.
PTE. Rodney Gido Ndunguru.
PTE. Fortunatus Wilbard Msofe.
PTE. Peter Muhiri Werema.
No comments:
Post a Comment