HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 12, 2013

Diwani wa Chadema atangaza vita na Mwenyekiti wa CCM na CUF

Na Bryceson Mathias
 
DIWANI wa Kata ya Mtibwa wilayani Mvomero wa Chama cha CHADEMA, Luka Mwakambaya, ametangaza vita na Mwenyekiti wa Chama Tawala (CCM), Seif Sekilojo, Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Mohamedi Kidevu, na Mtendaji wa Mji Mdogo wa Madizini, Saimon Muyogo, kwa kutengeneza mazingira ya Kulamba asilimia 20% ya fedha za MKUKUTA.
 
Mwakambaya alitangaza vita hiyo hadharani kwenye mkutano wa hadhara  uliofanyika J’mosi Agosti 10, mwaka huu, huku Mwenyekiti wa CUF Kindevu, akiwepo uwanajani hapo hapo akimuona na kumsimsikiliza .
 
Vita ya Mwakambaya na Viongozi hao, inatokana na kuwapotosha wananchi wa Mji huo kuhusu Maagizo ya Baraza la Madiwani ya Halmashauri ya Mvomero kwenye Kabrasha, kuhusu matumiza ya fedha za MKUKUTA zaidi ya Mil. 32/- zilizoamuliwa zitumike kumalizia miradi inayosuasua.
 
“Mimi ndiye Rais wa Kata ya Mtibwa. Nimegundua Paka akitoka Panya anatawala, hivyo sitakubali wakati huu wa Njaa Kali, wananchi wadanganywe na kuchangishwa Michango ya Miradi inayosuasua, wakati Madiwani tulishafanya maamuzi ya matumizi ya fedha hizo”.alisema Mwakambaya
 
Aliongeza, “Sipo tayari kuona wananchi wanachangishwa fedha zinazoitwa za maendeleo, kumbe mnawafanya wawalishe na kuwasomeshea watoto wenu! Nasema fedha hiyo ndiyo itakayotumika..Nilikataza wasilipe Ushuru na Michango na Mkuu wa Wilaya anajua hilo”.
 
Mwakambaya aliwafumbua macho wananchi kuwa, Serikali ya CCM Mji Mdogo wa Madizini inadaiwa zaidi ya Mil. 3/-, Kunke zaidi ya Mil.1/- na Kidudwe zaidi ya Mil.1/-, wakidai wamekopa Vifaa vya Ujenzi kwa matajiri wanataka walipe.
 
“Wananchi kataeni; watajua watakakopata fedha hiyo, wanataka kuwafanya Punda ili mchange muwalishie na kuwasomeshea watoto wao, na mimi sikubali fedha ya MKUKUTA iende huko, Patachimbika!” alishangiliwa Mwakambaya.
 
Aidha Mapema kwenye kikao cha Baraza Maendeleo la Kata (BMK), Wenyeviti wa Vijiji walikubaliana na kuridhia matumizi ya Fedha hiyo akiwemo Sekilojo, lakini huyo huyo    alikataa akidai CCM kimemwagiza akatae, na Kidevu akidai watakwenda Mahakamani, Mwakambaya akidai wanataka mwanya wa kuzifuja fedha hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages