HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 02, 2013

KCB BANK WAFUTURISHA JIJINI DAR

 BENKI ya KCB Tanzania inatarajia kufungua tawi jipya jijini Dar es Salaam mwezi huu, litakalokuwa maalum kwa ajili ya kutoa huduma za kibenki zinazofuata sharia za kiislamu
 
Akizungumza muda mfupi kabla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Moizz Mir alisema mahitaji ya huduma za kibenki zinayofuata sharia imekuwa ikikuwa kwa kasi katika nchi mbali mbali ulimwenguni ikiwamo Tanzania
 
Mkurugenzi huyo alisema kuwa, kutokana na mahitaji ya huduma hiyo hapa nchini benki yake ilianzisha huduma hiyo mwaka 2008 na kuongeza kuwa mahitaji yameendelea kuongezeka tangu kipindi hicho
 
“Kwa kutambua umuhimu wa huduma hii pamoja na kukwa kwa mahitaji, tumeamuamua kuanzisha tawi ambalo litakuwa malum kwa ajili ya kutoa huduma mbali mbali za kibenki zinazofuata sharia,” alisema
 
Mgeni rasmi katika hafala hiyo ambaye ni Rais mstaafu wa wawamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi aliipongeza benki hiyo kwa huduma hiyo kwa ajili ya waislamu huku akiwasisitiza waislamu kujitokeza kujiunga nayo ili kunufaika
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo Dk. Edmund Mndolwa Pili aliushukuru  Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania  kwa  kuungana na KCB bank katika hafla hiyo na aliwapongeza kwa kazi nzuri za kijamii na kidini wanazozifanya ikiwemo pamoja na kutoa ushauri wa kibenki kwa benki mbalimbali nchini ikiwemo KCB Bank katika kuunda, kusimamia  na kuuza huduma zinazofuata sharia.
 
“Napenda pia kuwapongeza kwa jitihada zenu zakusuluhisha migogoro mbalimbali nchini ili kudumisha amani ambayo ndicho kitambulisho kikuu cha nchi yetu ulimwenguni kote,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages