HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 02, 2013

KKKT DODOMA; WENGI WAGUSWA KUMCHANGIA NYUMBA YA ASKOFU NGOWO!

Na Bryceson Mathias, Dodoma
 
WAUMINI wengi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, wameguswa na kujitokeza kwa wingi kumchangia Ujenzi wa Nyumba ya Askofu Mstaafu Festo Daudi Ngowo ambaye amefumbwa kinywa na hasemi.
 
Katika Harambee rasmi iliyofanyika Jumapili iliyopita Julai 28, mwaka huu, Sharika nyingi za Mjini Dodoma zilivuka Malengo malengo yao waliyopangiwa na Uongozi wa Dayosisi, Majimbo, Sharika na Mitaa, ambapo Usharika wa Iringa Road uliongoza kwa kutoa Mil. 2/-.
 
Akizungumza na Gazeti la Upendo Askofu Msaidizi Samweli Mshana aliwapongeza Waumini wote wa Dayosisi kwa Ushirikiano Mkubwa wa Njia hii ya Kikristo, ambapo alisema Utandazaji wa Mbao za Dari (Blundering) umekwisha na leo (Jana) uwekaji wa Madirisha (Grill) unaanza mara Moja.
 
“Waumini na Watumishi wote kwa ujumla wao wanataka kuteka Baraka, na ni kweli tunakwenda kuziteka, kwa sababu waumini kila kona wamejguswa kujitolea kumsaidia Askofu wao (Ngowo) kwa hali na Mali, Jambo ambalo limetufurahisha sana Viongozi wa Dayosisi”.
 
Katika Harambee hiyo, Mafundi wa Utandazaji wa Umeme wa Kanisa Kuu (Cathedral) Dodoma na Ipagala KKKT walitolea bure kufanya kazi hiyo, huku Mwalimu wa Veta na Mzee wa Kanisa la Ipagala Mtalaam wa Ufundi Bomba, pia alijitolea kufanya kazi hiyo bure, na wengi walijitolea Malumalu (Tiles).
 
Aidha Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Amoni Kinyunyu, amewashukuru waumini wote kwa kujitoa, na amewaomba wachungaji, Wainjilisti na Ma-Parish workers wote, kuwakilisha fedha na Michango yote imfikie Kaimu Askofu Mkuu Mshana na Kamati ya Ujenzi wa nyumba hiyo, tayari kwa utendaji.
 
Hata hivyo Kamati ya Ujenzi, inakusudia hadi mwezi wa Septemba Mwaka huu Askofu Ngowo awe ameingia kwenye Nyumba hiyo, ili apumzike nyumanai pake kwa kazi nzuri ambayo amemfanyia Mungu aliyemuinulia watu wa kumsaidia.

No comments:

Post a Comment

Pages