HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 21, 2013

Mwenge uzimwe uwekwe Makumbusho ya Taifa?

Kupanga ni kuchagua!’
 
Na Bryceson Mathias
 
Kutokana na Matukio ya Uovu, Kashikashi, Karaha Vitisho na Usumbufu wanaoupata Wananchi kuhusu kuchangia mbio za Mwenge, wanasiasa wenye mtazamo chanya wanaona Mwenge Uzimwe ukawekwe Makumbusho ya Taifa.
 
Kauli za Mwenge uzimwe na kuwekwa Makumbusho ya Taifa, zinatokana na viashiria vingi vya uovu vinavyotokana na mwenge huo unapokimbizwa vijijini  na Mijini ambapo wananchi na wanasiasa walio wengi wanadai umepoteza lengo lililokusudiwa na waasisi wake.
 
Watanzania waliotoa mawazo wanadai, Manyanyaso, kukosekana kwa Haki, Vitisho, kukosekana Amani na Afya miongoni mwa Jamii dhidi ya Viongozi katika Mitaa, Vitongoji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mikoa na Taifa kwa sehemu kubwa mbio za Mwenge zinachangia.
 
Baadhi ya Viongozi mijini na vijijini wenye mapenzi mema na wananchi nchini, wametoa siri wakidai kipindi cha Mwenge kikifika, Wananchi wanakuwa na Mzigo mkubwa kwa sababu wanalazimishwa kutoa michango mingi kufanikisha mbio hizo.
 
Ijapokuwa wananchi wenyewe wanakuwa hawana hata mulo mmoja, lakini cha kushangaza wamekuwa wakitakiwa kuchangia Sh. 5,000/- hadi 10,000/-, na walalahoi wanaposhindwa basi wamekuwa wakilundikwa Lupango na wengine kunyang;anyway biashara zao ndogondogo.
 
Kutokana na kwamba nyakati hizo huwa ni nyakati za kuzindua Miradi mbalimbali, huwa kuna michango mingi inayoadaiwa ni ya Maendeleo ya kumalizia Miradi ambapo wananchi hukumbana na adhaa ambazo hufanywa na Watendaji wa Vijiji na Kata na kuwaacha Maskini.
 
Mbali ya Manyanyaso na Kero za michango inayowapelekea watu kufungwa, Maambukizi ya Magonjwa (Ukimwi) yamekuwa kichocheo kikubwa miongoni mwa Vijiji na Miji, ambapo Serikali huigharimu kutokana na uharibifu wa wanafunzi na Jamii.
 
Kwa msingi huo, Serikali kwa upande wake, huonekana kama inaangamiza nguvu kazi yake, na kwamba inapoamuru mwenge ukimbizwe, inatafsiriwa inapeleka maangamizo kwa watu wake, ingawa lengo ni kupeleka maendeleo, lakini uharibifu unakuwa Mkubwa zaidi ya tija.
 
Kingine kinacholalamikiwa na wananchi na viongozi wa Ngazi chini kuhusu Mbio za Mwenge, ni matumizi mabovu ya michango inayochangwa na wananchi, kwamba imekuwa ikiwasomesha na kuwalisha kama si kuwavisha watoto wa watendaji wa Vijiji Kata Tarafa Majimbo, Wilaya na Mikoa.
 
Ushahidi wa Vielelezo vinavyotolewa ni kwamba, Idadi ya fedha zinazochangishwa kila Kaya   kimaandishi huoneshwa wachache, lakini kimsingi wanaochangishwa huwa ni wengi ila taarifa za kiasi kinachopatikana zinachakachuliwa. Inahojiwa fedha hizo zinakwenda wapi?
 
Wakati mwenge mkoani Dodoma (shule ya Msingi Ipagala), kulizunduliwa Matundu mawili ya ya Vyoo vilivyokarabatiwa, lakini shule hiyo ina wanafunzi wanakaa chini. Gharama iliyofanikisha uzinduzi huo inatosha kutengeneza madawati ya shule nzima. je tunafikiri?
 
Agosti 19, Dodoama; Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Wilbroard Slaa aliulizwa kwenye Rasimu ya mabadiliko Katiba mpya, ni pamoja na Mbio za Mwenge kuondolewa maana hazina tija zaidi ya kuleta madhara ya ajali na maambukizi.
 
Dk. Slaa katika ufafanuzi wake alisema, kusudi lilolokusudiwa na Waasisi wa Mbio hizo, limekiukwa badala yake Mbio hizo imekuwa mitaji na vyanzo vya Ufisadi na kuwanufaisha watu wachache ambapo alisema, Mwenge unatakiwa Uzimwe na Ukawekwe kwenye Makumbusho ya Taifa, jambo lililoshangiliwa na wananchi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma hivi karibuni, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Susan Kaganda, alisema Watu tisa wamejeruhiwa katika ajali ya gari kwenye msafara wa mbio za Mwenge.

No comments:

Post a Comment

Pages