HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 06, 2013

Polisi amwandikia Makamu wa Rais Dk.Bilal, akipinga kufukuzwa kwa fedheha:

Na Bryceson Mathias
ASKARI Polisi (pichani) mwenye namba D5788D Koplo Patrice Masiko wa Upelelezi Wilaya ya Dodoma, amemwandikia Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipinga kufukuzwa kwa aibu Juni 24, 2011.
Katika barua yake ya Agosti 2, mwaka huu, Masiko anamuomba Makamu wa Rais Dk. Bilal, amsaidie kumhimiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, ampe Majibu ya rufaa ya Mashitaka ya Kijeshi yaliyosikilizwa tangu Novemba 30, 2010 hadi Juni 24, 2011.
Katika barua hiyo kwa Dk. Bilal, Masiko anasema, anamuombi amsaidie kumhimiza IGP ampatie majibu ya rufaa ya Mashitaka na Hukumu ya Kijeshi dhidi yake, yaliyosikilizwa na ZM Majunja na SSP-OCD Mpwapwa toka Novemba 30, 2010 hadi Juni 24, 2011.
“Julai 19, nilimwandikia IGP rufaa ya kupinga mwenendo mzima wa Mashitaka na Hukumu iliyotolewa lakini sikupata majibu. Agosti 16, 2011 nilimwandikia tena kukumbushia, lakini sijapata majibu.
“Tangu hapo mpaka leo sipati mshahara wala Posho kitendo ambacho ni Uonevu, Ukatili, Unyanyaswaji, na pia ni kinyume cha Sheria” ilisema sehemu ya barua hiyo ambayo gazeti hili linacho Kivuli chake.
Aidha Masiko ameorodhesha sababu Nane zilizopelekea kukata rufaa, ikiwemo kunyimwa nakala ya mashitaka kwa ajili ya utetezi, kutozingatiwa kwa PGO, 104 (4), PGO 106 (28) (C), Kukosa Imani na Msikilizaji, kutojulishwa tarehe ya Kesi, kutotendewa haki PGO 106 (24), kutopewa nafasi ya kujitetea na kuita mashahidi, kesi kuhukumiwa mkewe akiumwa, Mkutano wa Kizota 2010, na ushahidi wa PHQ.

No comments:

Post a Comment

Pages