HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 10, 2013

Ningekuwa Pindi Chana, Ningejiuzulu na kuiomba radhi Jamii!

Na Bryceson Mathias


Ingawa Waswahaili husema “Usipostaajabu ya Musa, utayaona ya Filauni, mbali ya  Mbwembwe Uongo, Uhuni na vurugu  zilizofanywa bungeni hivi karibuni, sasa watanzania tunaanza kusikia na kuyaona Maajabu ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Pindi Chana.

Katika hali isiyo ya kawaida, Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimetoboa Mwavuli uliokifunika CCM kuhusu vurugu za Katiba mpya uliofikiwa bungeni, ambapo  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Pindi Chana, alitaka kuwabebesha ADC mzigo usio wao.
 
Mbali ya Mwenyekiti wa ADC, Said Miraji kumsuta Chana, pia katika maelezo yake kimesikitishwa na kauli ya Mwenyekiti huyo kutaka kukibebesha dhambi na lawama isiyowahusu na kumtaka abebe imtafune kama msalaba wake badala ya kuwatwisha ADC.
 
Mwandishi wa Makala hii katika upekuzi amebaini, Chama cha Wananchi (CUF) visiwani Zanzibar kimemtaka, Rais Jakaya Kikwete, kutousaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013  ambayo sasa inaonesha kuingia Mdudu.
 
Licha Miraji kudai wamesikitishwa na kufadhaishwa na upotoshwaji wa makusudi uliofanywa dhidi ya kiongozi wao aliyeshiriki kutoa maoni juu ya muswada huo, wananchi wanahuzunishwa na ujasiri wa Chana kujigamba na kile alichowasilisha ingawa kinachoonesha watanzania wamedanganywa. 
 
Miraji alisema kauli iliyotolewa na Chana bungeni kuhusu ADC kuwakilishwa katika kamati yake si sahihi, kwani wao kama walivyokuwa waalikwa wengine walitoa maoni yao na si ya kuwawakilisha Wazanzibari kwa ujumla wao.
 
Tunajiuliza, hivi viongozi wanaotegemewa kuwa wakweli halafu hawasemi huo ukweli, wataendelea kuwadanganya na kuwapumbaza watanzania mpaka lini? Je wanadhani watu wa leo ni wale wa 1947, waliokuwa wakisema ipite kama alivyosema mchangiaji aliyetangulia?
 
Chana Kutaja kwamba ADC ni miongoni mwa vyama vilivyotoa maoni kwa niaba ya Wazanzibari, jambo hilo ni la kweli? Kama si la kweli, Chana kwa kufanya hivyo alikuwa na maana gani kwa Bunge na Watanzania kwa ujumla wao?
 
Ndiyo maana awali nimesema, ningekuwa Pindi Chana tena Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria, na Kamati yangu ikaonekana imefanya madudu yanayoendelea kujitokeza kwa namna ya kuipotosha jamii na Watanzania kwa Ujumla, kwanza Ningejiuzulu na ningewaomba radhi Watanzania kutunza Heshima yangu.
 
Katika moja ya kauliza za kumpinga Chana Miraji alisema kuwa kitendo kilichofanywa na Mwenyekiti wa Kamati (Chana) kinaweza kuihujumu ADC na kuisalitisha kwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla wao, jambo ambalo alisema hawawezi kulinyamazia wala kulifumbia Macho. 
 
Miraji alisema, “Ushahidi upo wa ADC kushiriki kama mdau katika kikao hicho, hivyo wanaopotosha ukweli kuhusu jambo hili waache mara moja na wanapojibizana bungeni wasitumie ADC kama ngao ya kujikingia,” alisema. 
 
Aidha alisema, ADC kama vyama vingine vya siasa na mdau wa muswada, ilipokea barua ya mwaliko kutoka kwa Katibu wa Bunge iliyosainiwa kwa niaba yake na Ruhilabake Julai 22, ikiwa na Kumb. Na. BA. 50/56/01/04.
 
Barua hiyo alidai iliwataka kutuma wawakilishi na ikafanya hivyo. Alisema katika uwakilishi huo walimtuma aliyewahi kuwa Mbunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Shoka Khamis Juma,  ambaye kwa asili ni Mzanzibari na alifuatana na, Mwamvita Mangupili,.
 
Ni rai yangu kuangalia, kwa viongozi wetu hawana tabia ya uwajibikaji wanapofanya mambo ya ovyo yaliyo wazi?
 

No comments:

Post a Comment

Pages